Pages

October 14, 2014

ANGALIA MKE WA KIGOGO AFIA GESTI.


MMH! Majanga! Mama mmoja aliyejulikana kwa jina la Juliet Gaison Komba (37), mkazi wa Mbagala Kuu, Temeke, Dar hivi karibuni amekutwa na mauti akiwa Gesti ya Kigoma, Mbagala Charambe, Dar.
Waombolezaji wakilia kwa uchungu kanisani.Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, mwanamke huyo ambaye mumewe ni kigogo mwenye cheo cha mkurugenzi wa kampuni moja ya usafirishaji jijini Dar, alikutwa na mauti baada ya kuingia kwenye gesti hiyo na mwanaume mmoja aliyedaiwa kuwa ni hawara yake licha ya kuwa na mume. 
Mmoja wa wahudumu wa gesti hiyo, Nickson John alisema siku ya tukio, mwanamke huyo na jamaa yake aliyevaa kofia maarufu kwa jina la kapelo, walifika kwenye gesti hiyo saa saba mchana.
Alisema: “Waliulizia chumba chao cha siku zote maana walikuwa wakifika kila wakati, nikawaambia kiko wazi.
Ndugu na jamaa wa karibu wakiomboleza msibani.
“Nilifuatana na mwanaume hadi kwenye chumba hicho namba 5, alilipia kisha kuzama na huyo mwanamke.“Saa kumi mwanaume alitoka, akaniambia anakwenda kutafuta chakula endapo mwanamke wake atahitaji kinywaji nimpe.
“Ilipofika saa kumi na mbili jioni, nilianza kuingiwa na hofu kwani yule mwanaume alikuwa hajarudi na mwanamke hakutoka kuhitaji kinywaji.“Niliamua kwenda kugonga mlango lakini hakuitika. Niliendelea kukaa kusubiri kama yule mwanaume atarudi lakini wapi!
Padri akiweka msalaba juu ya kaburi la marehemu Juliet Gayton Komba.
“Saa moja usiku nikiwa sijawaona, nikaenda kugonga kwa nguvu huku nikiita bila mafanikio, bosi wangu aliyelala chumba kingine alinisikia akaja.“Nilimweleza tatizo naye aligonga hakuna aliyeitika, tukazunguka dirishani kuchungulia, tukamwona mwanamke amelala kitandani lakini tulipata wasiwasi huenda alipatwa na tatizo.“Bosi wangu aliwapigia simu polisi, walifika na kuvunja mlango ambapo walimkuta mwanamke amekufa huku akitokwa damu mdomoni, waliuchukua mwili hadi Hospitali ya Wilaya ya Temeke kwa uchunguzi.”
Mume wa marehemu Bw. Deusi Komba.
Akaendelea: “Si mara yao ya kwanza kuja hapa, kwa mwezi waliweza kuja hata mara tano. Yule mwanaume hadi namba yake ya simu alinipa, ninayo.”
Kwa upande wake, Deusi Komba ambaye ni mume wa marehemu alipoulizwa kuhusu tukio hilo alikiri kutokea.Alisema asubuhi ya siku hiyo alimuacha marehemu nyumbani na kwamba hakuwa na mpango wa kutoka lakini aliporudi jioni hakumkuta na simu yake kila alipoipiga ilikuwa ikiita bila kupokelewa.
Juliet Gaison Komba (37) .Alisema ilibidi aende Kituo cha Polisi Maturubai kutoa taarifa na ndipo alipoelezwa kuwa, mkewe huyo anayemsaka amekutwa amekufa gesti.Marehemu huyo alizikwa Jumanne iliyopita katika Makaburi ya Mbagala Kuu, Dar na ameacha watoto watatu.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, (pichani) alipoulizwa alikiri kutokea kwa tukio na kusema uchunguzi unaendelea.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...