Dotto Mwaibale
SERIKALI
imesema itaainisha ukomo wa tozo kwa kila huduma inayotolewa kwa kila
ngazi ya kituo cha huduma ili kudhibiti gharama za huduma za afya
nchini.
Kauli
hiyo ilitolewa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid
Dar es Salaam wakati akizindua bodi mpya ya ushauri ya Hospitali binafsi
nchini.
Dk.
Rashid alisema hatua hiyo imekuja baada ya kuwepo kwa malalamiko kuhusu
huduma zinazotolewa na hospitali hizo hivyo hatua hiyo itasaidia
kuboresha mfumo na kuwatendea haki wananchi wanaotumia vituo vya
kutolea huduma za afya.
"Malalamiko
haya ni pamoja na huduma zisizo na ubora unaotakiwa na gharama
zinazotolewa kwa huduma hizo .Sheria iliyopo inatutaka kudhibiti bei ya
huduma hizi kwa kuzingatia malalamiko haya pamoja na matakwa ya sheria
yenyewe," alisema Dk. Rashid.
Hata
hivyo alibainisha kuwa licha ya kuwepo wa changamoto hizo huduma
zinazotolewa na hospitali za watu binafsi zimechangia katika mafanikio
yaliyopatikana katika kufikia malengo ya maendeleo ya milenia.
Kuhusu
bodi hiyo Dk .Rashid aliwataka wajumbe wapya wa bodi hiyo kufanya vikao
vya mara kwa mara vinavyolenga uboreshwaji wa utoaji wa huduma.Na
kuwataka kuendeleza utaratibu wa kusajili vituo vipya na kufupisha
usajili kwa kutmia muda mfupi kwa kutumia mfumo wa kielektroniki.
Alibainisha
kuwa wajumbe wa bodi ya awali iliyosimamiwa na Mwenyekiti Dk. Deo
Mtasiwa imesaidia kuboresha uwajibikaji wa wahusika hivyo kuboresha
huduma na imeokoa maisha ya wananchi wengi ambayo yangekuwa hatarini
endapo bodi isingetekeleza majukumu yake ipasavyo.
Alitaja
wajumbe wa bodi mpya kuwa ni Dk.Donan Mbando ambaye ni Mwenyekiti,
Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa mbeya Dk. Mpoki Ulisubisya, Mkurugenzi
wa Hospitali ya Bugando Profesa Chalres Majinge, Mkurugenzi wa Tiba na
Masuala ya Kiufundi (NHIF), DK. Frank Lekey.
Wajumbe
wengine ni Mkurugenzi Msaidizi- Hospitali za Umma na Binafsi Idara ya
Tiba Dk. Sijenunu Aaron, Mkurugenzi wa Association of Private Health
Facilities (APHTA), Mwakilishi wa Mkurugenzi, Christian Social Services
Comission (CSSC), Dk.Jane Kahabi na Mwanasheria Ofisi ya Mwanasheria
Mkuu wa Serikali Onorious Njole.
Waziri
wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Seif Rashid, akizungumza na wajumbe wa
bodi hiyo iliyomaliza muda wake na mpya wakati akizindua bodi hiyo Dar
es Salaam.
Mwakilishi
wa bodi mpya, Mkurugenzi wa Tiba na Masuala ya Kiufundi wa Mfuko wa
Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Dk.Frank Lekey akitoa neno la shukurani.
Kushoto ni Naibu Msajili Hospitali Binafsi Dk.Mahewa Lusinde
na Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, Dk.Mpoki Ulisubisya.
Waziri
wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Seif Rashid (kulia),akimkabidhi cheti
cha utumishi wa bodi hiyo,Profesa Bakari Lembariti. Katikati ni Mganga
Mkuu wa Serikali, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Dk.Donan
Mmbando. Vyeti hiyo walitunukiwa wajumbe wote waliomaliza muda wao.
Wajumbe
wa Bodi mpya wakiwa kwenye hafla hiyo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa
Tiba na Masuala ya Kiufundi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),
Dk.Frank Lekey, Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, Dk.Mpoki
Ulisubisya, Mwanasheria Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Onorius
Njole, Mkurugenzi Association of Private Health Facilities-APHTA na
Kaimu Mkurugenzi Msaidizi-Hospitali za Umma na Binafsi Idara ya Tiba,
Dk.Sijenunu Aaron.
Wajumbe
wa bodi iliyomaliza muda wake. Kutoka kulia ni Profesa .Bakari
Lembariti, Profesa Charles Majinge, Dk.Edda Vahahula, Dk.Jane Kahabi na
Dk.Eliuter Samky.
Mkutano ukiendelea.
Mkurugenzi
wa Tiba wa Wizara hiyo, Dk.Margareth Mhando na Mkurugenzi wa Idara ya
Uhakiki na Ubora, Dk.Mohamed wakiwa kwenye mkutano huo.
Katibu wa Bodi hiyo, Dk.Pamella Sawa akizungumza katika mkutano huo.
Kaimu
Mkurugenzi Msaidizi-Hospitali za Umma na Binafsi Idara ya Tiba,
Dk.Sijenunu Aaron akiteta jambo na Mkurugenzi Msaidizi wa Vituo vya
Umama na Binafsi na Mwakilishi wa Bodi ya Ushauri ya Hospitali Binafsi
Mkoa wa Dar es Salaam, Dk Ruth Suza.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Seif Rashid, akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi iliyomaliza muda wake.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Seif Rashid, akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi mpya.
No comments:
Post a Comment