Pages

September 28, 2014

WADAU GASTO NA FEDERICA WALIVYOMEREMETA JIJINI ARUSHA


Afisa Uhusiano  Mwandamizi wa Chuo cha Ufundi Arusha(ATC)Gasto Leseiyo akiwa ame ‘pose’ kwa picha na  Bibi harusi  Federica  Sikale baada ya kufunga pingu za maisha katika Kanisa Katoliki Parokia ya Roho Mtakatifu Ngarenaro Arusha jana na kufatiwa na sherehe iliyofanyika ukumbi wa Leons Garden Sakina.

Gasto Leseiyo na  Mke wake Federica  Sikale baada ya kufunga pingu za maisha katika Kanisa Katoliki Parokia ya Roho Mtakatifu Ngarenaro Arusha wakiwa katika picha ya pamoja na Mama wazazi .

Bwana harusi Gasto Leseiyo akisalimia wageni  kwenye ukumbi wa Leons Garden,Sakina jijini Arusha akiwa na   Mke wake Federica  Sikale baada ya kufunga pingu za maisha.

Bwana harusi Gasto Leseiyo na  Mke wake Federica  Sikale wakiwa na wapambe wao Endrick Fredick(shoto) na Lucy Fransis(kulia) kwenye ukumbi wa  Leons Garden Sakina.
Paroko akiwapongeza wanandoa baada ya misa
Bwana harusi Gasto Leseiyo na  Mke wake Federica  Sikale wakitoka kanisani baada ya misa ya ilifanyika jana.
Ndugu wa maharusi waliohudhuria misa ya ndoa

Bwana harusi Gasto Leseiyo na  Mke wake Federica  Sikale wakijumuika kusakata muziki na ndugu zao waliohudhuria sherehe hiyo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...