Pages

September 19, 2014

UONGOZI WA KAMPUNI YA NYUMBA KUBWA YA SERIKALI YA DUBAI ‘NAKHEEL’ WA TEMBELEA MAENEO YA MIRADI NA UWEKEZAJI WA ‘NHC’ KAWE,KUNDUCHI NA KIBADA.

AMkurugenzi wa Ubunifu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Issack Peter akimwelekeza jambo Mwenyekiti wa Kampuni ya Nakheel ambayo ndio kampuni kubwa ya Serikali Dubai ambayo ni wawekezaji wakubwa duniani katika sekta ya uendelezaji miliki, Rashid Ahmed Lootah wakati kiongozi huyo na ujume wake walipotembelea nyumba za mradi wa gharama nafuu Kibada, Dar es Salaam, Katikati ni Balozi Mdogo wa Tanzania Dubai, Mheshimiwa Omar Mjenga.

Mwenyekiti huyo na ujumbe wake wakiongozwa na Balozi Mjenga walikuwa kwenye ziara ya miradi mbalimbali ya NHC na Menejimenti ya Shirika la Nyumba la Taifa. (Picha zote za Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii cha Shirika la Nyumba la Taifa, NHC)BMkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akijadiliana jambo na Balozi Mdogo wa Tanzania Dubai, Mheshimiwa Omar Mjenga wakati wa ziara hiyoya leo.CMkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu, Balozi Mdogo wa Tanzania Dubai Mheshimiwa Omar Mjenga (kulia) na Mkurugenzi wa Ubunifu wa NHC, Issack Peter wakitembelea mradi wa nyumba za gharama nafuu za NHC Kibada sambamba na Mwenyekiti wa Kampuni ya Nakheel, Rashid Ahmed Lootah, , nyuma yake ni Mkurugenzi Mkuu wa Ujenzi wa Miradi wa Kampuni hiyo, Masood Al Zarooni na Injinia Fawzi Al Shah ambaye ni Mkurugenzi wa Udhibiti na Mipango Miji wa Kampuni hiyoEMwenyekiti wa Kampuni ya Nakheel, Rashid Ahmed Lootah, nyuma yake ni Mkurugenzi Mkuu wa Ujenzi wa Miradi wa Kampuni hiyo, Masood Al Zarooni na Injinia Fawzi Al Shah (Katikati) ambaye ni Mkurugenzi wa Udhibiti na Mipango Miji wa Kampuni hiyo wakisikiliza maelezo ya Mkurugenzi wa Ubunifu Issack Peter (Mwenye suti nyeusi).FMwenyekiti wa Kampuni ya Nakheel, Rashid Ahmed Lootah (kulia) akijadiliana jamo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu huku Mkurugenzi Mkuu wa Ujenzi wa Miradi wa Kampuni hiyo, Masood Al Zarooni akiwasikiliza.GMkurugenzi wa Ubunifu Issack Peter (Mwenye suti nyeusi) akijadili jambo huku Mwenyekiti wa Kampuni ya Nakheel, Rashid Ahmed Lootah na Mkurugenzi wa Uendeshaji Mikoa wa NHC, Raymond Mndolwa na Injinia Fawzi Al Shah wa Naheel wakifuatilia majadiliano hayo.HMkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu, Balozi Mdogo wa Tanzania Dubai Mheshimiwa Omar Mjenga, Mkurugenzi wa Uendeshaji Mikoa wa NHC, Raymond Mndolwa na Mwenyekiti wa Kampuni ya Nakheel, Rashid Ahmed Lootah wakijadilia jambo katika eneo la Kawe Tanganyika Packers.IMkurugenzi wa Ubunifu Issack Peter (Mwenye suti nyeusi) akijadili jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Ujenzi wa Miradi wa Kampuni ya Nakheel, Masood Al Zarooni na Injinia Fawzi Al Shah katika eneo la Tanganyika Packers Kawe, Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...