Pages

September 17, 2014

TANZANIA KUFAIDIKA NA MFUKO WA MPANGO WA MAENDELEO YA KIMATAIFA YA LFI


 

Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu kataka Wizara hiyo Dkt. Deogratius Mtasiwa alipokuwa katika mkutano na Katibu Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Fedha za Maendeleo ya Mitaji (UNCDF) nchini Judith Karl na wandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu kataka Wizara hiyo Dkt. Deogratius Mtasiwa (kulia) alipokuwa katika mkutano na Katibu Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Fedha za Maendeleo ya Mitaji (UNCDF) nchini Judith Karl (kushoto) na wandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam.
Katibu Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Fedha za Maendeleo ya Mitaji (UNCDF) nchini Judith Karl (kushoto) akiongea na wajumbe kutoka TAMISEMI na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam kuhusu Mpango wa Fedha wa Kidunia na Kitaifa (LFI). Kulia ni Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu kataka Wizara hiyo Dkt. Deogratius Mtasiwa.
Mtaalamu wa Ushauri wa UNCDF Peter Malika (katikati) akiongea na waandishi wa habari leo jijini dara es salaam kuhusu LFI na chini ambapo amesema kuwa lengo lake ni kutoa ushauri wa kitaalamu, fedha na namna ya kuchagua miradi yenye tija katika jamii ili wananchi waweze kujiletea maendeleo yao wenyewe na taifa kwa ujumla. Kulia ni Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu kataka Wizara hiyo Dkt. Deogratius Mtasiwa na kushoto ni Afisa Habari TAMISEMI Rebecca Kwandu. (Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)
Na Eleuteri Mangi – MAELEZO
Serikali ya Tanzania itafaidika kwa kupata fedha za maendeleo zaidi ya Sh. 46400 za kitanzania ambazo ni sawa na dola milioni 29 za kimarekani ili kusaidia miradi mbalimbali ya maendeleo nchini.
Kati ya fedha hizo, zaidi ya sh. milioni 41600 za kitanzania ambazo ni sawa na Dola za Kimarekani milioni 26 ni mkopo na sh. 4800 za Kitanzania ambazo ni sawa na  Dola milioni tatu ni msaada kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linalojihusisha na  Mfuko wa Maendeleo (UNCDF) nchini ambazo zinatarajiwa kunufaisha miradi mitano kwa miezi sita hadi tisa inayokuja.
Ili kufanikisha azma hiyo, Serikali kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa linalojihusisha na  Mfuko wa Maendeleo ( Capital Development Fund) wamezindua Mpango wa Kifedha wa Kidunia na Kitaifa (LFI) ambao utatekelezwa nchini kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2014 hadi 2017. Mradi wa LFI nchini unasaidia miradi 25 katika sekta za umeme, miundombinu vijijini, mawasiliano, viwanda na masuala ya usindikaji katika mikoa 10 ambapo mikoa ya Pwani na Kilimanjaro kupitia halmashauri za Kibaha na Same ni miongoni mwa halmashauri zinazonufaika na mradi huo.
Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu kataka Wizara hiyo Dkt. Deogratius Mtasiwa alipokuwa katika mkutano na Katibu Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Fedha za Maendeleo ya Mitaji (UNCDF) nchini Judith Karl leo jijini Dar es salaam.
Dkt. Mtasiwa amesema kuwa Serikali inajukumu la kutoa huduma za jamii kulingana na mazingira ya ndani ambapo jukumu hili linasimamiwa katika ngazi ya halmashauri wakati Serikali Kuu jukumu lake ni kupanga na kutoa sera zinazosimamiwa na kutekelezwa katika ngazi ya Serikali za Mitaa.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Fedha za Maendeleo ya Mitaji (UNCDF) nchini Judith Karl amesema kuwa ushirikiano uliopo kati ya Serikali ya Tanzania kupitia TAMISEMI umekuwa ni kiini cha kutekeleza mipango mbalimbali inayosimamiwa na UN.
Aidha, Judith amesema kuwa mpango wa LFI unalenga kuongeza uboreshaji wa rasilimali fedha kwa maendeleo ya kiuchumi kupitia mitaji na masoko ili kuweza kukuza na kufikia malengo ya maendeleo ya ndani ya nchi.

Naye Mtaalamu wa Ushauri  wa  UNCDF Peter Malika amesema lengo la LFI l ni kutoa ushauri wa kitaalamu, kifedha na namna ya kuchagua miradi yenye tija katika jamii ili kuwawezesha wananchi waweze kujiletea maendeleo yao wenyewe na taifa lao.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...