Pages

September 12, 2014

RADAMEL FALCAO ATAKA KUTENGENEZA UGWIJI MANCHESTER UNITED

Reds revolution: Louis van Gaal (C) prepares to unveil his final two summer signings Radamel Falcao (L) and Daley Blind (R) at Old Trafford

Mapinduzi ya mashetani: Louis van Gaal (katikati) akijiandaa kumtambulisha wachezaji wake wa mwisho katika usajili wa majira ya kiangazi, Radamel Falcao (kushoto) na Daley Blind (kulia) katika dimba la Old Trafford
RADAMEL Falcao amesema Manchester United watakapomsaini kwa mkataba wa muda mrefu baada ya kumaliza wa sasa wa paundi milioni sita kwa mkopo, anataka kukaa klabuni hapo kwa miaka mingi na kuweka historia Old Trafford.
Mshambuliaji huyo wa Colombia alitambulishwa sambamba na kiungo aliyesajiliwa kwa paundi milioni 14, Daley Blind jana alhamisi baada ya kufanya mazoezi kwa mara ya kwanza chini ya Louis van Gaal.
United wana chaguo la kumnunua Falcao kutoka Manaco majira yajayo ya kiangazi kwa dau la paundi milioni 52 na wamekubali kumlipa mshahara wa paundi lakini 2 na elfu 80 msimu huu.
Akizungumza kwa kuchanganya Kiingereza na Kihispania, Falcao alisema: "Nina matumaini ya kukaa Manchester United kwa miaka mingi na kutengeneza historia. Nilipokuwa FC Porto na Atletico Madrid siku zote nilikuwa napenda kujiimarisha na niliota kucheza timu kama hii. Sasa nataka kukaa hapa kwa miaka mingi".
Get shirty! Radamel Falcao (L) and Daley Blind (R) pose with the famous shirts as they are introduced at the Theatre of Dreams
Chukueni jezi zenu! Radamel Falcao (kushoto) na Daley Blind (kulia)  wakipozi na jezi zao wakati wa kutambulishwa Theatre of Dreams, Old Trafford
Staying power: Monaco striker Radamel Falcao revealed that he would like to stay at Manchester United for many years
Sitaki kuchomoka: Mshambuliaji wa Monaco, Radamel Falcao anataka kukaa Manchester United kwa miaka mingi

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...