TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
KUTOKA
OFISI YA KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA
TAARIFA
YA UKAMATAJI WA WATUHUMIWA WAWILI WAKIWA NA MADAWA YA KULEVYA AINA YA BANGI
MAGUNIA MANNE.
MNAMO TAREHE
23/09/2014 MUDA WA SAA 23:00 USIKU KATIKA MAENEO YA NDURUMA HALMASHAURI YA JIJI
LA ARUSHA, JESHI LA POLISI MKOANI HAPA KUPITIA KITENGO CHA KUZUIA MADAWA YA
KULEVYA TULIFANIKIWA KUWAKAMATA WATU WAWILI AMBAO NI LAIZER S/O MELAU (35) MKAZI WA ORKOKORA NA RICHARD S/O FANUEL (38) DEREVA NA MKAZI WA MIANZINI WAKIWA WANASAFIRISHA
MADAWA YA KULEVYA AINA YA BANGI MAGUNIA MANNE YENYE JUMLA YA UZITO WA KILOGRAMU
173 KWA KUTUMIA GARI AINA YA TOYOTA
COROLLA LENYE NAMBA ZA USAJILI T.
592 AAP.
MAFANIKIO HAYO YALIPATAKANA
BAADA YA WANANCHI AMBAO NI RAIA WEMA KUENDELEA KUWA KARIBU NA JESHI LA POLISI
AMBAPO WALITOA TAARIFA JUU YA TUKIO HILO NA JESHI LA POLISI MKOANI HAPA KUANZA
KULIFANYIA KAZI KWA KUWEKA MTEGO MAENEO YA NDURUMA.
MARA BAADA YA
KULIONA GARI HILO WALILISIMAMISHA NA WALIPOFANYA UPEKUZI WALIYAONA MAGUNIA HAYO
MANNE NDANI YA GARI HILO, KATI YA HAYO MATATU YALIKUWA KWENYE ‘’SEAT’’ YA
KATIKATI NA MOJA LILIKUWA KWENYE ‘’BOOT’’.
KATIKA MAHOJIANO WATUHUMIWA
HAO WALIKIRI KUHUSIKA NA TUKIO HILO NA WALISEMA KWAMBA, WALIKUWA WANAYAPELEKA
MKOANI TANGA. UPELELEZI WA TUKIO HILI BADO UNAENDELEA NA MARA UTAKAPOKAMILIKA
WATUHUMIWA HAO WATAFIKISHWA MAHAKAMANI. AHSANTENI
KWA KUNISIKILIZA.
IMETOLEWA
NA KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA
KAMISHNA
MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI
(SACP)
LIBERATUS SABAS
TAREHE
25/09/2014.
No comments:
Post a Comment