Ajali za
barabarani duniani hutokea kila uchao, na wahitaji wa damu wanazidi
kuongezeka huku idadi ya wachangia damu nayo ikizidi kushuka siku hadi
siku na kuleta hatari kwa maisha ya wahitaji.Kutokana na hali hiyo mji
wa Baoji nchini China uko kwenye harakati za uhamasishaji uchangiaji wa
damu kwa mtindo wa kipekee , kampeni ambayo imewekwa ni kwamba kama
unahitaji kujiunga na chuo,ukitaka kujifunza udereva na hata ukitaka
kuoa ama kuolewa sharti uchangie damu, kampeni ambayo imezua mjadala
mkubwa kwenye mitandao ya kijamii.
Sharia
hiyo mpya iliyotambulishwa katika jimbo la Shaanxi mjini,itaanza
kutumika rasmi wiki ijayo inawataka askari na wanachuo wa mwaka wa
kwanza kuchangia damu walau mara moja kwa mwaka .Wananchi wa China
wanaotaka kuomba leseni za udereva,wanaopokea vyeti vya uhitimu wa
mafunzo, wanaoajiriwa kwa mara ya kwanza, na wale wanaofunga ndoa kwa
msajili wa ofizi za mji wa Baoji wanapaswa kuchangia damu kwa lazima
kama mchango wao kwa jamii.
Taarifa
hii ilichapishwa katika mtandao na website ya mji huo wa Baoji, lakini
kampeni hii imekumbwa na changamoto ikiwemo wakaazi wa mji huo kuhoji
damu hiyo inayotakwa kwa mtindo huo wanahoji uchangiaji ukoje na damu
hiyo itatumika wapi, badala ya kuifikiria Zaidi sharia hiyo mpya.
Katika
jimbo la Pujiang lililoko Zheijang wao wameichukulia tofauti kampeni
hiyo na hivyo wanaongeza alama za ziada kwa wanafunzi wa sekondari ambao
wazazi na walezi wenye utamaduni wa kuchangia damu.
No comments:
Post a Comment