Mshindi wa taji la Redd’s Miss Tanzania Top
Model 2014, Jihan Dimachk (katikati) akipozi kwa picha na mshindi wa pili Doreen
Robert (wapili kulia), mshindi wa tatu Evelyn Baasa ambaye pia ni Miss Tanzania
Photogenic 2014 (wapili kushoto), mshindi wa nne, Lilian Timothy (kulia) na
Mshindo wa tano Nasreen Abdul, mara baada ya kushinda taji hilo jana ambapo Jihan
amekuwa mrembo wa pili kuingia katika nusu fainali za Miss Tanania 2014 baada
ya Miss Photogenic. Shindano la Miss Tanzania Top Mode lilifanyika katika ukumbi
wa Triple A jijini Arusha na kuwashirikisha warembo 30..Picha/Father Kidevu Blog
Warembo wakipita jukwaani wakiwa wamevalia nguo za mbunifu Zakia Disign wakati wa shindano hilo.
Washiriki wakipita jukwaani na
mavazi maridhawa kutoka Trecy Fashion ya jijini Arusha.
Jopo la majaji wakiwa katika meza yao tayari kwa kutoa hukumu kwa walicho kiona.
Wadau
wa urembo kutoka, Chuo cha Chuo Kikuu Iringa (Tumaini) na Makumira
jijini Arusha wakifuatilia shindano hilo ambapo mwenzao Martha John
alikuwa akitupa karata yake jukwaani.
Mwana dada Vanesa Mdee na kikosi kazi chake walishambulia jukwaa vilivyo wakati wakisindikiza shindano hilo usiku huu.
Wadau mbalimbali wa sanaa ya urembo na mitindo jijini Arusha wakiwa wamejumuika katika shindanohilo.
Mbunifu wa mavazi, Zakia akipozi kwa picha.
Mtangazaji wa kipindi cha
burudani cha Funika Base kutoka Radio 5 ya Mjini Arusha , Julius Kamafa ndiye
alikuwa mshereheshaji katika shindano hilo.
Mwanasheria
Machachari wa Jijini Arusha, Albert Msendo (kulia) akiwa na mkali wa
Bongo Fleva, Mwana FA wakifuatilia shindano hilo.
No comments:
Post a Comment