Pages

August 1, 2014

WAZIRI MAKALLA AKAGUA MIRADI YA VISIMA VYA MAJI MKURANGA


 Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla (kulia), akipata maerlezo kutoka kwa kiongozi wa Mafundi wa Kampuni ya CDM Smith, John Donoherth, kuhusu ujenzi wa kisima kilichopo Mkwalia Mkuranga ambacho ni moja kati ya visima 8 vinavyofanyiwa utafiti maji wilayani humo. Makalla alifanya ziara ya kukagua miradi ya maji wilayani Mkuranga mkoani Pwani leo. Pia alikagua mradi wa  kisima cha maji cha Nyamato chenye uwezo wa kutoa maji lita 26,000 kwa saa kitakachohudumia wakazi wa vijiji vya  Mvuleni, Nyamato na Kilimahewa.
 Waziri Makalla akiangalia mradi wa kisima cha Mkwalia ambacho kinafanyiwa utafiti
 Maji yakitiririka kwenye kisima hicho
 Makalaa akijadiliana jambo na Mkandarasi wa kisima hicho,John Donoherth
 Naibu Waziri Makalla akielezea namna Kisima kipya cha Nyamato kikianza kufanya kazi kuwa kitakuwa kinatoa lita 26,000 za maji kwa saa na kuhudumia sehemu kubwa ya wananchi wilayani Mkuranga, Pwani. Atakizindua kisima hicho mwanzoni mwezi ujao kitakapowekwa pampu iliyoagizwa Afrika Kusini. Kulia ni Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Nyamage, Abdallah Kiyewehe ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya maji kijijini hapo.
 Mama mkazi wa Kijiji cha Mvuleni, wilayani Mkuranga akielezea mbele ya waziri jinsi wanawake wa eneo wanavyopata taabu ya kuata maji karibu umbali wa Km 5, na kuonesha furaha ya kupata kisima hicho kitakachowaondolea adha waliyokuwa wanaipata.
 Eneo la Kisima cha Nyamato kilichogauliwa. Kisimamhicho kinasubiri pampu tu ili kianze kufanya kazi.
 Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla akihutubia mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Mvuleni baada ya kukagua kisima cha maji cha Nyamato, wakati wa ziara yake wilayani Mkuranga leo.
 Sehemu ya umati mkubwa wa wananchi ukimsikiliza Makalla akihutubia kwa kuwaeleza mikakati ya Serikali ya kuwaboreshea wananchi sekta ya maji., ambapo  zimetengwa zaidi ya Bilioni moja kwa ajili ya wilaya hiyo.
 Wananchi wakisikiliza kwa makini hotuba ya Makalla
 Katibu wa Kamati ya Maji ya Mradi wa Nyamato, Ali Salum akielezea jinsi mradi wa Nyamato unavyosuasua kuzinduliwa, akidai anayesababisha hivyo ni Mkandarasi wa mradi huyo ambaye hatoi taarifa yoyote juu ya ucheleweshwaji huo.
 Mkandarasi wa mradi wa maji wa Nyamato, Jamila Chibwana wa Kampuni ya Mac Consultant  akitoa majibu ya ucheleweshwaji wa mradi huo, ambapo alisema moja ya sababu zilizosababishwa ni kutopewa fedga za ujenzi kwa wakati na uagizaji wa pampu kutoka Afrika Kusini.
Makalla akiagana na wananchi baada ya mkutano kumalizika. SOURCE: KAMANDA WA MATUKIO BLOG

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...