Mwanamuziki
Mkongwe hapa nchini,almaarufu kama Mzee Njenje akizungumza machache
mbele ya wasanii mbalimbali wa bongofleva waliofika nyumbani kwake
Sahare,nje kidogo ya jiji la Tanga,kumjulia hali kutokana na maradhi
yake yaliyokuwa yakimsumbua kwa muda sasa.
Mzee
Njenje amewaasa wasanii hao ambao amekiri wazi kuwa wanafanya vizuri
katika anga ya muziki wao,kupata muda mwingi wa kupumzika ikiwemo na
suala la kutoendekeza masualaua ya anasa kama vile ulevi,ngono na
mengineyo ambayo huchangia kuporomoka kwa wasanii wengi,amesema kuwa
Muziki wa sasa una ushindani mkubwa hivyo kila msanii anapaswa kujituma
kwa namna anayoona inafaa ili kutimiza malengo yake sambamba na
kuitangaza nchi kwa ujumla.
Wasanii wa Muziki wa Kizazi kipya,Rachael na Linah wakiwa wamepozi katika picha ya ukumbusho na Mzee Njenje.
Msanii wa muziki wa Kizazi Kipya,Alli Kiba akizungumza jambo na Mzee Njenje.
Mzee
Njenje akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wasanii wa muziki wa
kizazi kipya watakaotumbuiza jioni ya leo kwenye tamasha la Fiesta 2014
linalofanyika kwenye uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga,Wasanii hao
walikwenda kumsabahi mkongwe huyu wa Muziki hapa nchini,Nyumbani kwake
Sahare,nje kidogo ya jiji la Tanga ambako ndiko anaendelea kupata
matibabu yake ya maradhi yaliyokuwa yakimsumbua kwa muda sasa,Mzee
Njenje amesema kuwa kwa sasa anamshukuru Mungu anaendelea vizuri na afya
yake inazidi kuimarika kadiri ya siku zinavyozi kwenda.
Baadhi
ya Wasanii mbalimbali ambao Watatumbuiza kwenye tamasha la Fiesta jioni
ya leo ndani ya uwanja wa Mkwakwani ,wakiwasili nyumbani kwa Mzee
Njenje,Sahare,nje kidogo ya jiji la Tanga kumjulia hali.Picha zote na
Michuzi Jr-FIESTA TANGA
No comments:
Post a Comment