Wananchi wa kijiji cha Luvuyo kata ya Madope wakimpokea mbunge wao Deo Filikunjombe kwa maandamano |
Wananchi wa Luvuyo wakimsikiliza mbunge wao Deo Filikunjombe |
Mbunge wa jimbo la Ludewa akiwahutubia wananchi wa Luvuyo mara baada ya kuzindua ujenzi wa barabara ya Luvuyo - Njombe |
Na Francis GodwinBlog
WANANCHI
wa kijiji cha Luvuyo kata ya Madilu wilaya ya Ludewa mkoani Njombe
ambao awali walitaka kuhamia wilaya ya Njombe kutokana na Halmashauri ya
wilaya ya Ludewa kuwatelekezea barabara ya Luvuyo – Njombe wamempongeza
mbunge wao Deo Filikunjombe kwa kuwajengea barabara hiyo na kubadili
uamuzi wao wa kuhamia Njombe.
Wakizungumzakatika
hafla ya mbunge Filikunjombe kuzindua ujenzi wa barabara yenye urefu wa
kilometa zaidi ya 6 inayojengwa kwa zaidi ya milioni 52 ,walisema kuwa
awali walipata kuandika barua katika uongozi wa Halmashauri hadi kwa
waziri mkuu wakiomba kuhamia wilaya ya Njombe kutoka na kijji hicho kuwa
kama kisiwa kutokana na ubovu wa barabara .
Mmoja
kati ya wananchi hao Apudencia Lugome alisema kuwa wananchi hao
walifikia hatua ya kuandika barua ya kutaka kijiji hicho kuwa sehemu ya
wilaya ya Njombe kutokana na viongozi wa wilaya ya Ludewa kushindwa
kuwatekelezea maombi yao ya ukarabati wa barabara ya kijiji hicho toka
nchi ipate uhuru Kwani alisema kuwa mbali ya kujengwa kwa barabara ya
Njombe – Ludewa ila wao katika kijiji hicho barabara hiyo ilikuwa si
msaada kwao zaidi ya ile ya Luvuyo – Njombe ambayo hutumia kusafirisha
mazao yao na ni tegemeo katika usafiri hivyo kitendo cha Halmashauri ya
Ludewa kupuuza kilio chao ni kuwafanya wananchi hao kujisikia kama wapo
katika kisiwa .
Hivyo
alisema hatua kutoka na hali hiyo wao wenyewe wananchi walilazimika
kuchangishana fedha kiasi cha Tsh 50,00 kila mmoja na kupata kiasi cha
Tsh milioni 3.6 kwa ajili ya kuanza kutengeneza maeneo korofi kabla ya
mbunge wao kufika katika mkutano wake na kuamua kuchukua jukumu ya
kujitolea kujenga barabara hiyo yote .
“Tunashukuru
sana mheshimiwa mbunge wetu na jembe kwa wana Ludewa kwani toka nchi
yetu ipate uhuru Ludewa hatujapata kuwa na mbunge makini kama wewe hivyo
hatuna sababu ya kuhangaika na mtu mwingine mwaka 2015….kwani mwenye
kutatua kero zetu zaidi yako hakuna “
Huku
diwani wa kata hiyo Godfrid Mhagama wa kata ya Madope akieleza kuwa
sababu ya wananchi hao kufanya maandamano na kumpokea kwa usafiri wa
ng’ombe ni kutokana na heshima kubwa ambayo mbunge huyo ameionyesha kwao
wana kata ya Madope hasa wananchi wa kijiji cha Luvuyo .
Alisema
kuwa barabara hiyo imekuwa kero kiasi cha wananchi hao kuwakimbiza
watendaji wa Halmashauri ambao walifika katika kijiji hicho kwa ajili ya
kuhamasisha shughuli za kimaendeleo.
“Kweli
suala hili kwetu limetuumiza sana kichwa ilifika sehemu wakuu wa idara
walikuwa hawafiki katika kijiji hiki kutokana na wananchi kuwa na jazba
iliyotokana na ubovu wa miundo mbinu na ahadi zisizotekelezeka za
Halmashauri yetu”
Katibu
wa itikadi na uenezi CCM mkoa wa Njombe Onolatus Mgaya mbali ya
kumpongeza mbunge huyo na wananchi kwa kuunganisha nguvu zao bado
aliwataka wananchi hao kutunza barabara hiyo ambayo kukamilika kwake ni
ukombozi mkubwa kwao .
Alisema
kuwa wapo baadhi ya viongozi wamekuwa wakiangalia misaada inayotolewa
na Mbunge huyo kwa macho matatu ambapo baadhi hujikuta wakiiba na
kufanya ni mali yao binafsi kitu ambacho si kizuri bali wananchi
washirikiane na viongozi hao kuhakikisha wanailinda na kuisimamia
misaada wanayopewa iliiweze kuwanufaisha wote
“…Nampongeza
sana Mbunge kwa misaada mbali mbali aliyotoa kwa wananchi wake kwani
amejitahidi kuweza kutatua kero mbali mbali zinazowasumbua wananchi
katika sekta ya afya, elimu ,m iundombinu na kilimo, naomba tuitunze na
itumiwe na wananchi wote,"alisema Mgaya
Huku
Filikunjombea mbali ya kuzindua ujenzi wa barabara hiyo pia alikabidhi
msaada wa bati 200 ya geji 28 mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya ujenzi
wwa nyumba ya mganga wa Zahanati ya Luvuyo na ujenzi wa vyumba vya
madarasa katika shule ya msingi katika shule za msingi kijijini hapo pia
toroli na spendi kwa ajili ya kikundi cha vijana wanaojishughulisha na
uoteshaji miti kijijini hapo bado aliwataka kuendeleza umoja zaidi .
Kwani
alisema iwapo wananchi hao wataendelea kujitolea zaidi yeye kama mbunge
wao atazidi kuwwaunga mkono na kuwahakikishia kuwa kamwe hatawaangusha
katika utendaji kazi wake na kuwa siku zote anaamini kuwa mwwajiri wake
ni mpiga kura na si vinginevyo.
"
Ndugu zangu wana Luvuyo nawapenda sana baada ya kuja wiki iliyopita hapa
na kufanya mkutano kweli nilivutiwa sana na jitihada zenu ndio maana
nilikubali kuwasaidia kujenga badaraba hii kwa zaidi ya Tsh milioni 52
ila nawahakikishia fedha hizi hazijatoka mfukoni mwangu ila kutokana na
kuishi na watu vema nimewaomba mitambo nja mafuta ya kuja kusaidia
ujenzi huu baada ya kuvutika na jitihada zenu"
No comments:
Post a Comment