Wakongwe wa Klabu ya Real Madrid
ya nchini Hispania wakipiga picha za kikundi cha ngoma kilichokuwa
kikiwatumbuiza mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro kabla
ya kuelekea Mlima Kilimanjaro.
Wachezaji
wakongwe wa Klabu ya Real Madrid wakiwa katika picha ya pamoja na
watumishi wa TANAPA mara baada ya kumaliza zoezi la matembezi mafupi ya
kupanda Mlima Kilimanjaro.
Waziri
wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Dk. Fenela Mukangara akitoa
cheti cha ushiriki kwa mchezaji Ruben De La Red wa Klabu ya Real Madrid
mara baada ya kumaliza zoezi la matembezi mafupi ya kupanda Mlima
Kilimanjaro.
Meneja
Mawasiliano wa TANAPA Pascal Shelutete akikabidhi moja ya fulana za TANAPA kwa mchezaji.
wakali hao wa zamani wa Real Madrid wakiwa katikati ya msitu wa Mlima Kilimanjaro.
Eneo la Maporomoko ya Maji ambapo wachezaji wakali hao wa zamani wa Real Madrid walifanikiwa kufika Mlimani Kilimanjaro.
Meneja
Mawasiliano wa TANAPA Pascal Shelutete (mwenye fulana nyeupe na miwani)
akiongoza msafara wa wakali hao wa zamani wa Real Madrid kukwea Mlima Kilimanjaro.
No comments:
Post a Comment