Pages

August 7, 2014

FARM AFRICA YAWANUFAISHA WAKULIMA MKOA WA MANYARA,YATIA FORA MAONESHO YA NANENANE NJIRO

Ofisa masoko wa shirika la Farm Africa, Rahel Pazzia (kulia) akiwa na baadhi ya wakulima wa ufuta wa Wilaya ya Babati Mkoani Manyara jana, katika banda la Farm Afrika kwenye maonyesho ya wakulima nane nane kanda ya kaskazini, yanayofanyika viwanja vya Themi jijijni Arusha.

Watanzania wenye asili ya bara Asia wakipewa maelezo ya ubora wa mafuta ya ufuta kwenye banda la shirika la Farm Africa, katika maonyesho ya wakulima nane nane kanda ya kaskazini, yanayoendelea kwenye viwanja vya Themi jijini Arusha.

Mkulima wa ufuta wa Kijiji cha Ngolei Wilayani Babati Mkoani Manyara, Costante Martin, akiwa na zana ya kilimo iitwayo Coster Planter, ambayo aliibuni mwenyewe kwa kuwezeshwa na shirika la Farm Africa, hapa akiwa kwenye la Farm Africa katika maonyesho ya kilimo nane nane kanda ya kaskazini, yanayofanyika viwanja vya Themi jijini Arusha.

Emmanuel Stephano mkazi wa Kijiji cha Zeloto Wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara, hapa akiwa na miche aliyootesha kwenye banda la shirika la Farm Africa, katika maonyesho ya kilimo nane nane kanda ya kaskazini, yanayofanyika viwanja vya Themi jijini Arusha.

Ofisa miradi na masoko wa shirika la Farm Africa, kwa upande wa msitu wa Nou unaowanufaisha wakazi wa vijiji 33 vya Wilaya za Babati na Mbulu Mkoani Manyara, Hakam Mohamed akiwa na Philemon Lawrent (kulia) wa Kijiji cha Boboa wilayani Mbulu na Joseph Kufo wa Kijiji cha Bermy Wilaya ya Babati, wakiwa katika banda la Farm Afrika jana, kwenye maonyesho ya wakulima nane nane kanda ya kaskazini, yanayofanyika viwanja vya Themi jijijni Arusha.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...