Pages

August 2, 2014

BREAKING NEWS: BASI LA HOOD LAUA ARUSHA





Watu 2 wamekufa baada ya basi la Hood kwenda Mbeya kugongana na Hiace eneo la Kilala, Arusha asubuhi hii na watu 14 wajeruhiwa huku hali ya  Taarifa zaidi baadaye.
 
 

 Muonekano wa basi la Hood kwenda Mbeya baada ya kugongana na Hiace eneo la Kilala, Arusha mapema  leo.
 Wananchi wakiwa wamekusanyika baada ya basi la Hood lililokuwa linaelekea mkoani Mbeya  baada ya kugongana na Hiace eneo la Kilala, Arusha.
 Muonekano wa Hiace hiyo kwa mbele baada ya ajali.




Kwa mujibu wa Mganga Mkuu wa Hospitali ya wilaya ya Halmashauri ya Meru,mkoani Arusha,Dk Azizi Msuya amesema waliofariki dunia ni watu wawili ambao ni Jumanne Mohamed na Anaret Sabas aliyefariki dunia wakati akipelekwa kwa matibabu kwenye hospitali ya mkoa ya Mount Meru.

Amesema hali ya Grace Wilson ni mbaya sana kutokana na majeraha aliyoyapata kichani na kuwataja  majeruhi wa ajali hiyo waliolazwa katika hospitali ya mkoa kuwa ni watu watano ambao ni Leginald Gustadi,Abbas Jumanne na Nicholaus Laurence,Aminiel Mbise.

Wengine waliolazwa katika hospitali ya Wilaya ya Meru ni ambao hali zao zinaendelea vizuri ni Judica Peter,Philipo Kilembi,Kilamba Kiyayenga,Dominic Yasanta,Asifiwe Abeli,Witness  Elias na Rogathe Kiungai.


 

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...