Naomba unipe nafasi nitoe maoni
yangu kuhusu Urahi pacha nikijbu maoni yaliyoandikwa kwenye gazeti la mwananchi
na bwana Humphrey Polepole. Maoni yake yamenishangaza sana na mtu huyu
anaonekana ana hujuzi kidogo katika mambo ya uandishi na ameamua kutumua ujuzi
wake kudanganya watu kuhusu swala hili la urahia pacha kwa watanzania.
Napenda iheleweke kwamba urahia
pacha sio kitu kigeni Tanzania. Kimsingi na kimazingira tanzania inaruhusu urahia pacha. 1.kwa watanzania
wote walio na wazazi wenye urahia tofahuti mpaka watakapofikisha miaka ishrini
na moja. 2.Kwa wanzanzibar wanye urahia wa zanzibar na urahia wa Tanzania.
Tatizo
lililopo sasa ni watanzania wanataka
wanufaike na urahia wa nchi nyingine pia na sio watu wengine wanufaike na urahia
wa Tanzania. Hofu inayowekwa na wasiopenda maendeleo ya watanzania ni
kudanganya kuwa wakongo, wamarekan, wasomali
na wengineo ndio watanufaika na urahia pacha. Kitu ambacho sio kweli
mkongo atakapotaka kuwa rahia wa tanzania lazima aombe kupitia uhamihaji ya
tanzania urahi huo. Na kira nchi inasheria zake kuhusu uraia wa kuomba, nchi kama tanzania inabidi huwe
umekaa ndani ya nchi kwa miaka isiyopungua kumi.na bado uchunguzi utafanywa
kuhusu tabia zako na huko ulikokuwa kabla ya kupewa urahia wa Tanzania. Kwani
hata ukikamilisha taratibu zote hizo bado idara ya uhamiaji inaweza kukukatila
kuwa rahia wa Tanzania . Sasa ofu ya kusema wageni wengi watanufaika na urahia wa tanzania. Inatoka wapi.
KINACHOOMBWA
NA WATANZANIA WENGI NI KUWA NA HAKI YA KUPATA URAHIA WA NCHI NYINGINE BILA
KUPOTEZA URAHI WAKO WA TANZANIA. HUWE NA URAHI PACHA. HII LITAKAPORUHUSIWA
WATAKAONUFAIKA NI WATANZANIA NA SIO WAGEN. WATANZANIA TUNATAKA URAHI PACHA,
HATUOMBI SERIKALI IVUNJE MASHARIT YA KUPATA URAHI WA TANZANIA KWA WATU WASIO
WATANZANIA.
Sasa
naomba nijibu hoja za bwana Humphrey Polepole.
1.Mr. Humphrey
Polepole anasema kwamba ”Tuchukue mfano mwingine,
sasa tuna sera ya kuhudumu katika jeshi kisheria kwa vijana wetu kama sehemu ya
kujenga ushupavu na kuimarisha uzalendo wao, tukiwa na uraia pacha tujiandae
kuwa na Warundi, Wakongo, Wamarekani, Wakenya na Wasomali JKT tukiwafundisha
uaminifu, utii na namna ya kuipenda Tanzania kwa moyo wote hata na ikibidi
mpaka tone la mwisho la damu yao.”
Hoja hii aina msingi wowote,
kama kwa sheria za sasa za Tanzania zinaruhusu kijana aliyezaliwa na wazazi
wenye urahia tofahuti kuwa na urahia wa nchi zote mbili hadi atakapofikishe
miaka 21. Hii inamaana kwamba atakuwa ameshamaliza JKT akiwa na urahia wa nchi
mbili tofahuti. Na kama akiamua kuacha utanzania na kuchukua urahia wa mzazi
asieyekuwa mtanzania bado atakuwa alishapitia mafunzo ya JKT na kumaliza. Sasa
hilo la JKT halina maana yeyeyote.
2.Bwana huyu aneendelea kwa
kusema ”Zaidi ya yote, uraia
pacha unavunja msingi wa haki ya usawa kwa sababu katika taifa moja, raia
wanawekwa katika mafungu, wale wenye uraia wa zaidi ya nchi moja, ambao
wanakuwa na haki zote nchini na haki zaidi kwingineko dhidi ya wale wenye uraia
mmoja, ambao wana haki zote za hapa nchini pekee, lakini wote wako sawa nchini”
Hapa anajifunua zaidi kuonyesha
kuwa yeye ana wivu binafsi kwa wale wanaoweza kupata urahia pacha kwa kuwa
watunufaika huko kwingine. Kwasababu urahia pacha hautampa mtu haki ya kufunja sheria za nchi au
kupewa uwaziri au ubalozi na kumnyima yule mwenye urahia mmoja. Kwani tumeona
watu wa nchi mbalimbali waliovunja sheria tanzania wakishikwa na kufunguliwa
mashitaka na kufungwa tanzania bila ya kuwa na urahia wa tanzania, kwa makosa waliyofanya
Tanzania. Hivyo uwe na urahia pacha au usiwenao, wote tutafuhata sheria moja
ndani ya tanzania. Na tutakuwa na haki sawa na hakuna atakayetuweka kwenye
makundi labda huyu bwana mwandishi mr. Polepole
3.Bwana
Polepole anasema ” Mapendekezo haya yalizingatia kuwa
nchi itakapotambua uraia wa nchi mbili, haitakuwa na msingi wa kikatiba na
kisheria wa kuwazuia raia wa nchi nyingine kubaki na uraia wao wanapokuwa raia
wa kuandikishwa wa Tanzania kwa kuzingatia kuwa Jamhuri ya Muungano inapakana
na nchi nane na italeta changamoto ya usalama na ulinzi.”
Rahia wa
nchi nyingine anapojiandisha kuwa rahia wa Tanzania anakuwa rahia wa tanzania
wa kuandikishwa, Huyu ni Rahia wa nchi nyingine sio mtanzania. Hapa sisi
tunazungumzia Mtanzania kupata urahia wa nchi nyingine, nazani hajaelewa somo.
Ina maana kuwa wewe ni mtanzania lakini huwe na haki kubaki na urahia wa
tanzania na kuweza kupata urahia wa nchi nyingine. Kama ni swala la usalama
hizo nchi zitakazompa mtanzania urahi wao ndio zinatakiwa ziwe na wasiwasi
kwamba anaweza kufanya upelelezi kwa niaba ya Tanzania na sio vinginevyo. Kama
tunampa mkongo urahia wa tanzania tunakuwa na wasiwasi anaweza kupeleleza kwa
ajili ya kongo sasa mtanzania marekani atapeleleza kwaajili ya tanzania huko
aliko na sio vinginevyo.
Unajuha
swala hili hawa wenye wivu binafsi wanataka kuwatisha watu wengine kwa faida
zao wenyewe. Wanaposema maslahi binafsi dhidi ya maslai ya nchi wana maana gani.
Kwani hao binafsi ni kina nani na nchi ni kina nani. Tatizo lililopo ni kuwa
wapo watu wengi waliozoea rushwa na njia za ujanja ujanja kupata riziki
wanaojuha kuwa hawa wanaotaka urahia pacha wengi wao ni watu waliosoma nje na
hawatohi rushwa na watakapopewa urahia pacha watarudi nyumbani kufanya kazi kwa
moyo wote hivyo kuchukua nafasi za wezi na wala rushwa ndio maana mnaona vita
inakuwa kubwa kwa swala hili la urahia pacha. Hakuna hasara yeyeyote
atakayopata mwananchi wa kawaida au nchi kwa kuruhusu urahia pacha ni faida tu
kwa walio nao na rahia wema wote.
Mimi sizani
kama Bwana Humphrey Polepole anajuha siri za serikali au jinsi ya kulinda
usalama wa nchi hii kuliko Rais Jakaya Kikwete, au Waziri Benard Membe.
Waliosema waziwazi kwamba urahia pacha utaleta faida kwa tanzania na kuhinua
uchumi wa nchi kwa kiasi kikubwa.Sizani kama rais wetu angkubali hilo kama
anaona litahatarisha usalama wa nchi hii kwa namna yeyeyote hile.
Unajua
watanzania wengi walio nje ya nchi wana uwezo wa kati. Biashara watakazokuja
kufanya tanzania bila hofu ya kuzulumiwa watakapokuwa na utanzania wao zitawanufahisha
watu wa hali ya chini. Kwa mfano, Mtu atakuja kujenga nyumba,i wakati anajenga,
atanunua vifaa vya ujenzi hapo nyumbani na atatumia mafundi ujenzi ambao ni
wananchi wa kipato cha chini kujenga nyumba hiyo. Hao atawalipa na wao watapata
pesa za kusomesha watoto wao. Watakaopata hasara ni hawa wakina Humphrey
Polepole, wanawatumia hawa mafundi na hawataki kuwalipa pesa zao kwasababu
mafundi hawatakwenda kwao tena.
Kwa kifupi
hawa wanaopinga urahia pacha ndio wanamasilahi binafsi, na hawataki wananchi
wanufaike na faida za urahia pacha. Wananchi hamkeni na ungeni mkono urahia
pacha kama anavyofanya rais wetu na wengine wengi walio na masilahi ya kweli
kwa taifa na sio binafsi kama Mr polepole na waliomnunua atoe makala hii kwenye
gazet lake la mwananchi. Kichwa ni chako kitumie kuhamua vizuri kwa faida ya
Taifa lote. Mnufahishe Polepole au imefika wakati na sisi wote tunufahike.
Ahasante.
NYAGA NYAGA
No comments:
Post a Comment