Pages

July 5, 2014

SHEIKHE ALIYELIPULIWA KWA BOMU WAKATI AKILA DAKU ARUSHA, ATOBOA SIRI YA TUKIO BAADA YA POLISI KUZUBAA KUCHUKUA TAHADHARI.

 
 Matukio ya milipuko ya mabomu yameendelea kuuandama mkoa wa Arusha ambapo hapo jana majira ya saa 5 usiku katika eneo la Majengo ya chini jijijni Arusha kumetokea mlipuko wa bomu linalosadikiwa kuwa ni la kutengenezwa, nyumbani kwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Answar Suna Youth Center Shekh, Sudi Ali Sudi.

Tukio ambalo limesababisha watu wawili kujeruhiwa vibaya na kusababisha uharibifu wa mali katika nyumba ya mkurugenzi huyo.


Ni majeruhi wa tukio hilo la mlipuko wa bomu ambalo limetokea jana usiku nyumbani kwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Aswar Suna Youth Center Shekh Sudi Ali Sudi na Muhad Husen wakizungumza kwa tabu wakati walipokuwa wakielezea namna tukio hilo lilivyotokea.


Tukio ambalo limetokea wakati watu hao wakiwa wanajiandaa kula daku, mara baada ya kuvunjwa kwa kioo cha dirisha, na watu wasiojulikana kisha kurusha ndani kitu kinachasadikika kuwa bomu na kusababisha mlipuko mkubwa uliowasababishia majeraha.


Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Liberatus Sabas amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa tukio hilo limetokea muda mfupi baada ya taarifa za Shekh huyo ambazo amezitoa kwa jeshi hilo kuwa lipo kundi la watu ambalo limetishia kumdhuru kutokana na msimamo wake katika masuala ya imani yake.


Aidha kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mulongo na Mbunge wa Jimbo hilo Godbless Lema wamesema ipo haja ya viongozi wa dini na taasisi zake kuangalia namna nzuri ya kumaliza migogoro yao na kujiepusha na matumizi ya njia zisizokuwa sahihi katika kutatua migogoro ili kulinda amani ya mkoa na taifa kwa ujumla.


Tukio hili la mlipuko wa bomu linatajwa kuwa la tano kutokea jijini Arusha baada ya tukio la kutupiwa bomu katibu wa BAKWATA Mkoa wa Arusha mwaka 2012 , na kufuatiwa na matukio ya milipuko Katika Parokia ya Yosefu Mfanyakazi iliyopo Olasiti, Mkutano wa CHADEMA Katika viwanja vya Soweto na lile la mlipuko katika baa ya Arusha Night park.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...