Timu
ya taifa ya Arggentina imepokelewa kwa shangwe na maelfu ya watu
waliotaka kuwapongeza wachezaji wao, kuanzia uwanja wa ndege. Wanandinga
hao walishuka kutoka kwenye ndege maalum iliyokuwa imenakshiwa kwa
rangi za timu hiyo ikiwa na maandishi yaliyomaanisha 'Asante Argentina'
kwa lugha ya kwao.
Wachezaji hao walipita kwenye mitaa wakiwa ndani ya mabasi maalum huku kukiwa na mapokezi makubwa kuwahi kushuhudiwa.
Argentina
iliingia fainali za kombe la Dunia 2014, na kushindwa kutimiza ndoto
yao ya kutwaa kombe hilo kwa kufungwa na timu ya Ujerumani kwa bao moja.
No comments:
Post a Comment