Na Shaffih Dauda
KOCHA
wa Timu ya taifa ya Tanzania, Mholanzi, Mart Nooij aliamua kuwaanzisha
washambuliaji wanne katika mechi dhidi ya Msumbuji, kuwania kupangwa
hatua ya makundi ya kusaka tiketi ya kucheza fainali za mataifa ya
Afrika, AFCON, mwakani nchini Morroco.
Mbwana
Ally Samatta, Thomas Ulimwengu, John Bocco `Adebayor` na Mrisho Ngassa,
wote kwa pamoja walianza katika sare ya 2-2 ndani ya uwanja wa Taifa,
jinini Dar es salaam dhidi ya `Black Mambas`.
Lengo
la Nooij lilikuwa ni kushambulia kwa nguvu ili kupata mtaji mkubwa wa
mabao kabla ya mechi ya marudiano itakayopigwa wiki mbili zijazo mjini
Maputo nchini Msumbiji.
Lakini
kwa mtazamo wangu, niliona mapungufu juu ya namna kocha Nooij
alivyowapanga washambuliaji hawa. Ulimwengu na Ngassa walicheza pembeni,
Samatta na Bocco walisimama katikati.
Mimi naona ingekuwa na tija kama Thomas angecheza katikati kuliko kucheza pembeni ili kupata ubora wa timu.
Kwa
timu ilivyoanza yeye alikuwa kulia, katikati alikuwa Mbwana Samatta na
John Bocco, kushoto alicheza Mrisho Ngassa na wakawa wanabadilishana.
Lakini
mimi naona ingekuwa na tija zaidi kama Thomas Ulimwengu angesimama
katikati na John Bocco, halafu samata akawa anashambulia kutoka pembeni
upande wa kushoto, halafu Mrisho Ngassa ashambulie kutoka kulia.
Kwasababu kwa aina ya uchezaji wa Ulimwengu, walipokuwa wanamuweka
pembeni walikuwa wanampatia ugumu.
Alikuwa
analazimika apige chenga, apige pasi kutoka eneo alipo, lakini yeye sio
aina ya mchezaji wa hivyo vitu, yeye sio mtu wa vitu, yeye ni mtu wa
kuwekewa mpira ili awe na chaguo moja tu, kupiga au kupasia karibia na
goli ili kumpa mwenzie afunge, na hapo unaweza kuona ubora wa Thomas
Ulimwengu.
Kama
Ulimwengu angekuwa katikati ingekuwa ni vizuri zaidi kucheza mipira
mirefu waliyokuwa wanacheza akina `Cannavaro` dakika za kipindi cha
kwanza. Mara nyingi mipira hii mabeki wa Msumbiji walikuwa wanaicheza,
kwasababu John Bocco pamoja na umbile kubwa, mrefu, lakini sio mzuri
kupambana, ni mwepesi, kwahiyo ni mara mia nane angekuwepo Thomas
Ulimwengu, kwasababu ni mtu mwenye nguvu na jinsi mwili wake ulivyo
angeweza kupambana nao na kutoa mianya kwa akina Ngassa, Samatta au
Bocco mwenyewe kufungwa.
Hii
ni kwasababu mabeki wa Msumbiji wangelazimika kuokoa mipira hovyo, na
ingedondoka maeneo ambayo wengine wangeokota baada ya mikikimikiki ya
Ulimwengu.
Halafu
kingine, ile mipira, Ulimwengu angekimbia nayo katoka katikati na
kutanua kwenda pembeni. Hii ingetoa nafasi kwa akina Ngassa au Samatta
kutegemeana mpira unaenda upande upi.
Mabeki
wangelazamika kwenda kukimbiza na kuacha nafasi katikati, na kwasababu
yeye ana kasi angewahi ile mipira na kupiga krosi ambazo zingeweza
kufungwa na wenzake kwasababu katikati pale pangeachwa wazi kutokana na
mebeki kwenda pembeni kumkimbiza Ulimwengu.
Lakini
ilikuwa ni ngumu kwa Ulimwengu kutokea pembeni na kupiga mipira vizuri
kwasababu yeye hana uwezo wa kumiliki mpira vizuri, sio mtu wa kuchezea
mpira kama akina Ngassa au Samatta mwenyewe.
Unajua
Thomas Ulimwengu, Mbwana Samatta, John Bocco wote ni washambuliaji wa
kati, lakini wanatofautiana ujuzi na aina ya uchezaji.
Kama
mimi ningekuwa kocha na ningetaka kuwatumia wote kwa wakati mmoja, mara
mia nane, huyu Thomas Ulimwengu angesimama katikati, halafu Jonh Bocco
au Samatta angeenda pembeni.
Lakini
mimi ningependa zaidi Mbwana Samatta atokee pembeni upande wa kushoto,
kwasababu ana uwezo, ana kasi, na anaweza kupiga chenga na kutafuta
`engo` ya kupiga mpira. Anaweza kupiga chenga, akarudi na kuuzungusha.
Kuthibitisha
pointi yangu hiyo, kuna wakati Samatta alikwenda pembeni, alipiga pasi
mbili ambazo almanusura zisababishe goli. Alipiga krosi moja ambayo
alipigwa kichwa na John Bocco, lakini kipa akacheza.
Akapiga
krosi nyingine ambayo beki alitoa ikawa kona. Kwahiyo, kwayeye kucheza
pembeni ilikuwa na faida zaidi kuliko Thomas Ulimwengu.
Chanzo: shaffihdauda.com
No comments:
Post a Comment