Pages

July 21, 2014

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA ASHIRIKI MKUTANO WA TATU WA UMOJA TAASISI ZA MAGEREZA BARANI AFRIKA, MAPUTO MSUMBIJI


image_3
Rais wa Jamhuri ya Watu wa Msumbiji, Mhe. Dkt. Armando Guebuza(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Taasisi za Urekebishaji(Magereza) Barani Afrika pamoja na Washiriki Wengine wa Mkutano mara baada ya kufungua rasmi Mkutano wa Tatu wa Umoja wa Taasisi za Urekebishaji Barani Afrika, Maputo Msumbiji(wa Nne kushoto mstari wa pili) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(wa kwanza kushoto) ni Rais Mstaafu wa Msumbiji, Joaquim Chisasano(wa kwanza kulia) ni Kamishna wa Magereza Nchini Zambia, Percy Chato(wa tatu kulia mstari wa mbele) ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Namibia, Raphael Hamunyela(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

image_1
Baadhi ya Washiriki wa Mkutano wa Tatu(03) wa Umoja wa Taasisi za Urekebishaji(Magereza) Barani Afrika wakifuatilia Majadiliano ya Mkutano huo uliofanyika hivi karibuni Maputo, Msumbiji(wa kwanza kulia) ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Tanzania, John Casmir Minja(wa kwanza kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Uganda, Dkt. Johnson Byabashaija(mstari wa nyuma) ni Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza Nchini Tanzania wakifuatilia mjadala katika Mkutano huo wa Kimataifa.
image_2
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi Nchini Tanzania, Profesa Sifuni Mchome akiwasilisha Mada ihusuyo Urudiaji wa Vifungo Magerezani kwa Wahalifu(Recividism) katika Mkutano wa Tatu wa Umoja wa Taasisi za Urekebishaji(Magereza) Barani Afrika uliofanyika hivi karibuni Maputo, Msumbiji.
photo
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Tanzania, John Casmir Minja akichangia Mada katika Mkutano wa Tatu(03) wa Umoja wa Taasisi za Urekebishaji(Magereza) Barani Afrika uliofanyika hivi karibuni kuanzia July 14 – 17, 2014 Maputo, Msumbiji.
image
Maafisa na Askari Magereza wa Msumbiji wakimsikiliza Mgeni rasmi, Rais wa Jamhuri ya Watu wa Msumbiji, Mhe. Dkt. Armando Guebuza(hayupo pichani) katika ufunguzi wa Mkutano wa Tatu(03) wa Umoja wa Taasisi za Urekebishaji(Magereza) Barani Afrika uliofanyika Maputo, Msumbiji.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...