Mwandishi Wetu,Arusha
DIWANI wa kata ya Themi jijini Arusha,Milance Kinabo amenusuru shule
ya msingi Engira iliyopo jijini hapa,isifungwe, kutokana na adha
wanayoipata wanafunzi ya kutokuwa na vyoo kufuatilia choo kilikuwepo
kubomoka baada ya kukabidhiwa miaka miwili iliyopita na mfuko wa
maendeleo ya jamii nchini TASAF .
Aidha diwani huyo ameahidi kusaidia bila kutegemea wafadhili katika
kutatua kero mbalimbali zinazozikabili shule za msingi zilizopo
katika Kata hiyo,huku akitoa wito kwa wazazi kuhakikisha wanawahimiza
watoto wao kwenda shule na kuachana na utoro .
Akizungumza muda mfupi baada ya kukabidhi vifaa mbalimbali vya ujenzi
kwa ajili ya matundu kumi ya choo kilichobomoka katika shule
hiyo,alisema msaada huo ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi aliyoitoa ya
kuinua elimu katika Kata yake.
Aliongeza kuwa uongozi wa shule hiyo ulitoa taarifa kwake juu ya
kubomoka kwa choo hicho cha shule , kilichojengwa miwili iliyopita na
kusababisha adha ya muda mrefu kwa wanafunzi ,ambapo walilazimika
kujisaidia kwenye choo kingine ambacho pia ni kibovu.
Kinabo alimhakikishia mwalimu mkuu wa shule hiyo,Simon Siara, wakati
akimkabidhi vifaa hivyo kwamba hata kubali shule yeyote katika kata
yake ikabiliwe na changamoto itakayosababisha wanafunzi kukwama
kimasomo,ambapo aliahidi kutumia hata rasilimali zake kumaliza kero
yoyote inayohusu wanafunzi.
‘’mimi ni mwanasiasa ila sifanyi hivi kwa lengo la kujipatia
umaarufu,ispokuwa najaribu kuisaidia serikali kupunguza kero za msingi
ili watoto wapate ufaulu mzuri na si vinginevyo’’alisema Kinabo.
Diwani huyo aliahidi kuendelea kutatua kero zinazoikabili shule hiyo
pamoja na shule zingine zilizopo katika kata hiyo ikiwemo ya kuchangia
gharama za malipo ya umeme na maji pamoja na mishahara ya wlinzi wa
shule,kero ambayo inasumbua shule nyingi jijini hapa .
Mwalimu mkuu wa shule hiyo,alieleza kuwa halimashauri iliwaandikia
barua ya kuzitaka shule zote za kata katika jiji
malipo ya mlinzi wa shule tofauti na hapo awali walikuwa wakilipwa na
halimashauri .
Ama kwa upande wake, mwalimu Siara alisema kuwa, shule hiyo
inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo kutokuwepo na uzio wa shule
unaosababisha wanafunzi kutoroka ama kuvamiwa na vibaka ,
halikadhalika wazazi katika shule hiyo kutokuwa na mwamko wa kuchangia
maendeleo ya shule.
Siara aliwataka wadau mbalimbali kuchangia shule zenye changamoto ya
kimaendeleo, kwani tangu serikali ifupe michango mashuleni ,baadhi ya
shule zimeshindwa kujiendesha kutokana na kutokuwa na vyanzo vya
mapato .
Mwalimu mkuu huyo alikabidhiwa mifuko 8 ya sementi,Milango 10,Bomba za
maji 14,Sinki nne za matundu ya choo,kaomeo za milango na vifaa
vingine mbalimbali vya ujenzi.
No comments:
Post a Comment