Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea,
Mathias Chikawe (Kulia), akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya
CCM Kata ya Nditi, Wajumbe wa Mabaraza ya Jumuiya zote za CCM Kata,
Viongozi wa Dini na Wajumbe wa Baraza la Wazee katika Kata hiyo ya Nditi
wakati alipofanya ziara katika kata hiyo iliyopo Wilaya ya Nachingwea
mkoani Lindi. Waziri Chikawe alitoa mabati 100 kwa ajili ya ujenzi ya
Ofisi Kuu ya CCM katika Kata ya Nditi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea,
Mathias Chikawe (Kulia), akimkabidhi jezi za timu sita za mpira wa
miguu Afisa Mtendaji wa Kata ya Nditi, Patrick Mwasambungu kwa ajili ya
kuzikabidhi timu hizo zilizopo katika Kata hiyo katika Jimbo la
Nachingwea mkoani Lindi. Waziri Chikawe pia alitoa mabati 100 kwa ajili
ya ujenzi ya Ofisi Kuu ya CCM katika Kata hiyo ya Nditi. Mbunge huyo wa
Nachingwea yupo jimboni mwake kwa ajili ya kufanya ziara ya kuzungumza
na viongozi wa CCM katika ngazi mbalimbali.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea,
Mathias Chikawe (Kushoto), akikiangalia kifusi cha mchanga kwa ajili ya
ujenzi wa Ofisi ya CCM Kata ya Mnerongongo ambayo ipo katika hatua ya
mwisho kukamilika ujenzi wake. Katika ujenzi wa ofisi hiyo, Waziri
Chikawe alitoa mabati 100 ambayo tayari yameezekwa. Mbunge huyo wa
Nachingwea yupo jimboni mwake kwa ajili ya kufanya ziara ya kuzungumza
na viongozi wa CCM katika ngazi mbalimbali.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea,
Mathias Chikawe (Kushoto), akikagua ujenzi wa Ofisi ya CCM Kata ya
Mnerongongo ambayo ipo katika hatua ya mwisho kukamilika ujenzi wake.
Katika ujenzi wa ofisi hiyo, Waziri Chikawe alitoa mabati 100 ambayo
tayari yameezekwa. Mbunge huyo wa Nachingwea yupo jimboni akifanya ziara
ya kuzungumza na viongozi wa CCM katika Kata za Wilaya za Nachingwea
mkoani Lindi. Picha zote na Felix Mwagara.
No comments:
Post a Comment