LUIZ Felipe Scolari mambo yamemdodea kabisa baada ya usiku huu kuchapwa mabao 3-0 na Uholanzi.
Ushindi
wa Uholanzi ni zawadi kubwa kwa Louis Van Gaal ambaye ameiongoza kwa
mara ya mwisho timu hiyo na sasa anaenda kuungana na klabu yake ya
Manchester United.
Van
Gaal aliyekuwa na malengo ya ubingwa amefanikiwa kushinda nafasi ya
tatu katika michuano ya mwaka huu ya kombe la dunia baada ya kupigwa kwa
mikwaju ya penati na Argentina katika mchezo wa nusu fainali.
Katika
michuano ya mwaka huu, Van Gaal hajafungwa mchezo wowote ndani ya
dakika 90. Mechi pekee aliyofungwa ni ile ya penati dhidi ya Argentina.
Thiago
Silva ambaye hakucheza mechi ya nusu fainali alimuangusha kwenye eneo
la hatari, Arjen Robben mnamo dakika ya 3 na mwamuzi Djamel Haimoudi
(Algeria)alitoa penati iliyofungwa na Robin Van Persie kwa shuti la
mguu wa kushoto.
Robin Van Persie akifunga bao la kwanza kwa mkwaju wa penati
Beki
ghali zaidi duniani, David Luiz alifanya makosa makubwa yaliyosababisha
Daley Blind aifungie Uholanzi bao la pili katika dakika ya 16.
Jamani majanga tena: Julio Cesar akiwalaumu mabeki wake baada ya Daley Blind kuifungia Uholanzi bao la pili.
Wakati
Brazil wakihangaika kupata angalau bao la kufutia machozi, mabeki kama
kawaida wakiongozwa na Silva walifanya makosa na kumuacha Wijnaldum
afunge bao la tatu katika dakika za nyongeza.
Mabadiliko aliyofanya Van Gaal ya kumtoa kipa Jasper Cillessen na kumuingiza Michel Vorm katika dakika za lala salama, yanamaanisha Van Gaal ameweza kuwatumia wachezaji wote 23 wa kikosi chake.
No comments:
Post a Comment