Kwa mara
nyingine katika kipindi cha maisha yake ya soka, Luis Suarez ameingia
tena kwenye headlines kwa kumng’ata mchezaji mwenzie uwanjani.Kwenye
mchezo wa mwisho wa makundi kati ya Uruguay vs Italy, zikiwa zimebakia
dakika 9 mchezo kuisha ulitokea utata mkubwa wakati Suarez na Chiellini
walipokumbana katika maeneo ya penalti
Beki huyo wa Italia alilalamika wakati kwa refa kwamba alikuwa ameng’atwa na akajaribu kumwonyesha alama.
Wakati wachezaji wa Italia walipokuwa wakiendelea kulalamika, Uruguay wakapata kona.
Suarez alipiga pasi nzuri naye Godin akafunga bao hilo la ushindi.
Mpaka unamalizika Uruguay walikuwa washindi, na kuungana na Costa Rica kwenda hatua ya 16 ya michuano hiyo.
Wakati
huo huo Italy iliungana na England iliyomaliza mechi zake za makundi kwa
kutoka sare ya 0-0 na costa Rica – kufungasha virago kurudi nyumbani
zikishindwa kufuzu kwenda hatua ya pili.
Uruguay sasa itacheza na Colombia wakati Costa Rica ikikutana na Ugiriki kwenye hatua ya 16 bora.



إرسال تعليق