Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.
Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China,
Li Yuanchao, wakati alipowasili Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo juni
23, 2014 akiongozana na Ujumbe wake kwa ajili ya mazungumzo. Li
Yuanchao, yupo nchini kwa ziara ya siku sita.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akimkaribisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Li Yuanchao, wakati
alipowasili Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Juni 23, 2014 akiongozana
na Ujumbe wake kwa ajili ya mazungumzo. Li
Yuanchao, yupo nchini kwa ziara ya siku sita. Wa pili (Kulia) ni Balozi wa Tanzania, nchini
China, Luteni General Abraham Shimbo.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa
katika mazungumzo na Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Watu wa China, Li Yuanchao, wakati alipowasili Ofisini kwake Ikulu jijini
Dar es Salaam, leo June 23, 2014. Li Yuanchao, yupo nchini kwa ziara ya siku
sita.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (wa pili
kulia) na baadhi ya Mawaziri wake, akiwa katika mazungumzo na Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Watu wa China, Li Yuanchao, aliyeongozana na ujumbe wake wakati alipowasili Ikulu jijini Dar es Salaam,
leo Juni 23, 2014 kwa ajili ya mazungumzo.
Li Yuanchao, yupo nchini kwa ziara ya siku sita.
Baadhi ya
Mawaziri waliofika katika mazungumzo hayo Ikulu jijini Dar es Salaam, na baadhi
kusaini mikataba na watu wa China.
Waziri wa
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenella Mukangara (kulia) akisainiana
mkataba na Naibu Waziri wa Wizara ya Biashara ya Watu wa China, Li Jinzao, wa
Makabidhiano ya gari la matangazo la Shirika la Utangazaji la TBC,
yaliyofanyika mapema mwaka huu. Shughuli hiyo ya kutiliana saini imefanyika leo
Juni 23, 2014, Ikulu jijini Dar es Salaam, ikishuhudiwa na Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Li
Yuanchao.
Naibu Katibu Mkuu
wa Wizara ya Fedha, Dorothy Mwanyika, (kulia) akisainiana mikataba miwili na
Naibu Waziri wa Wizara ya Biashara ya Watu wa China, Li Jinzao, ya makubaliano
ya ushirikiano wa Kitaalamu utakaoiwezesha China kuwapa mafunzo Wanariadha wa
Tanzania nchini China na wa makubaliano ya awamu ya tatu ya Ushirikiano wa
kiufundi baada ya China kusaidia na kukamilisha Ujenzi wa Uwanja wa Taifa. Shughuli
hiyo ya kutiliana saini imefanyika leo Juni 23, 2014, Ikulu jijini Dar es
Salaam, ikishuhudiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Li Yuanchao.
No comments:
Post a Comment