Timu
ya Kagondo FC imejipatia Alama tatu muhimu kwenye Mtanange wao dhidi ya
timu ya Buhembe FC leo kwenye Uwanja wa Kaitaba Bukoba Mjini kwenye
Michuano ya Kombe la Kagasheki. Bao hilo la pekee lilifungwa na Mchezaji
namba tisa Mgongoni Abduratif Khamis katika kipindi cha kwanza dakika
37. Kipindi cha kwanza kilimalizika kwa bao hilo 1-0 na kipindi cha pili
timu zote mbili hakuna iliyoziona nyavu za mwezake timu licha ya
kushambuliana mara kwa mara. Mwamuzi alipuliza kipenga dakika 90
kumaliza mtanange huo na Timu ya Kagondo FC wakiibuka na ushindi huo wa
bao 1-0. Mapema leo Mchana Timu ya Nshambya na Kibeta ziliumana na timu
zote mbili zilimaliza mtanange kwa sare ya bila kufungana kwa kutoka
0-0. Kesho Ligi hii inaendelea tena kwa siku ya nne na kutakuwepo na
michezo miwili, Mapema ni Nyanga vs Kitendaguro na Jioni saa 10:00 ni
Wagonga Nyundo "Ijuganyondo Vs Kahororo".
Kikosi cha Timu ya Kagondo Fc
Kipute kilianza kwa Timu ya Buhembe kwa kasi sana
Kila Mtu na wake!
Wachezaji
wa Timu ya Kagondo Fc wakishangilia bao lao lililofungwa na Abduratif
Khamis katika dakika ya 37 kipindi cha kwanza. kulia ni kipa wao nae
alikuja kuwapongeza!!!
Mchezaji wa Kagondo aliumia, Watoa huduma ya kwanza wakimpa msaada wa kumtoa nje ya uwanja kwa matibabu
Kipa
wa Kagodo chupuchupu afungwe bao hapa katika kipindi cha pili. Kipindi
cha pili hakuna aliyeziona nyavu za mwenzake bao hilo lilidumu mpaka
dakika za mwisho
Hatari: Kipa wa Kagondo Fc akidaka mpira wa Kona
Kipindi
cha Pili dakika za mwishoni Timu ya Buhembe FC ilipata kona mbili
lakini haikuweza kusawazisha bao, licha ya kuliandama lango la wenzao
Kagondo Fc.
No comments:
Post a Comment