Kaimu
Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege la Air Tanzania (ATCL), Kapteni
Milton Lazaro (katikati) akipeana mkono na Meneja wa Kanda wa
Interair, Angelo Cossi mara baada ya kuzungumza na waandishi wa habari
(hawapo pichani) juu ya makubaliano yaliyosainiwa kati ya shirika la
ATCL na shirika la Interair la Afrika ya Kusini, yatakayowezesha kuwepo
na safari tatu kwa wiki kati ya Dar es Salaam na Johannesburg Afrika ya
Kusini. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Biashara wa ATCL Bw. Juma Boma
(kushoto). .
Kaimu
Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege la Air Tanzania (ATCL), Kapteni
Milton Lazaro (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo
pichani) jijini Dar es Salaam jana kutangaza makubaliano yaliyosainiwa
kati ya shirika lake na shirika la Interair la Afrika ya Kusini,
yatakayowezesha kuwepo na safari tatu kwa wiki kati ya Dar es Salaam na
Johannesburg Afrika ya Kusini. Wakishuhudia kushuto ni Meneja wa Kanda
wa Interair, Angelo Cossi na Kaimu Mkurugenzi wa Biashara wa ATCL Bw.
Juma Boma (kushoto)
======= ====== ========
SHIRIKA
la Ndege la Taifa la Air Tanzania (ATCL) limesaini mkataba wa
ushirikiano na kampuni ya Interair ya Afrika Kusini, itakayowezesha
shirika hilo kuwa na safari tatu kwa wiki kati ya Dar es Salaam na
Johannesburg, Afrika ya Kusini ikiwa ni kama ratiba ya mwanzo.
Taarifa
hiyo imetolewa siku chache tu baada ya mashirika hayo mawili kusaini
makubaliano ya kufungua soko la kitanzania kwa Interair na kulifufua
soko la Afrika ya Kusini kwa shirika la Ndege la Air Tanzania kwa
kupitia safari zitakazofanyika siku za Jumatatu, Jumatano na Ijumaa,
ikiwezeshwa na ushirikiano huo.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika ofisi za makao makuu ya ATCL jijini Dar
es Salaam jana, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa ATCL, Kapteni Milton Lazaro
alisema ushirikiano huo na Interair ni sehemu ya mkakati madhubuti wa
kuboresha shirika hilo, kama siyo kwa safari za moja kwa moja basi
kupitia ushirikiano wa aina hiyo, ili kuweza kurejesha huduma za shirika
hilo katika njia zote lililokuwa likiruka, likianzia Afrika ya
Kusini.
“Kwa
kutumia ndege za Interair, abiria wetu sasa watakuwa na uwezo wa
kusafiri kwenda na kutoka Johannesburg katika siku zifuatazo; itawasili
jijini Dar es Salaam kila Jumatatu na kuondoka kwenda Johannesburg
Jumanne, kuwasili Dar es Salaam Jumatano na kuondoka siku hiyo hiyo,
kuwasili Dar es Salaam Ijumaa na kuondoka kwenda Johannesburg siku ya
Jumamosi,” alisema.
Kapt.
Lazaro alibainisha kuwa mashirika hayo mawili sasa yanatoa fursa kwa
wasafiri kutoka nchi hizo mbili kuyafikia masoko, wanaotaka kutumia na
kupata uzoefu wa siku kuu za kipekee wanazo kuwa wakizisoma kuhusu
Afrika ya Kusini au Tanzania, na pia kutoa fursa za ongezeko la
ushirikiano wa kibiashara na kidiplomasia.
“Kwa
kupitia makubaliano haya mapya, tuna uhakika kuwa ratiba itakidhi haja
kwa wasafiri wote katika sehemu hizi mbili, na kutoa chanzo cha mapato
kitakacho changia katika ukuaji wa shirika la Air Tanzania, Sekta ya
Utalii Tanzania na uchumi wetu wa ndani,” alisema Kapt. Lazaro. Aliongeza
kuwa ATCL katika siku za usoni itatanua safari zake mpaka Arusha,
Zanzibar, Mwanza, Mbeya, Comoros na baadae katika maeneo mengine yote
inayofanyia shughuli zake.
Kwa
upande wake, Meneja Interair wa Kanda ya Afrika Mashariki, Bw. Angelo
Cossi, alisema: “Ushirikiano na Air Tanzania ni muungano nzuri kwa
sababu ya faida itakayopatikana ambayo itafaidisha mashirika haya
mawili.
“Shirika
la Interair la Afrika ya Kusini ni moja kati ya mashirika ya ndege
nchini Afrika ya Kusini yanayomilikiwa kibinafsi yenye mafanikio.
Shiriki hili, mwanachama wa Chama cha Kimataifa cha Usafiri wa Anga
(I.A.T.A), na Chama cha Mashirika ya Ndege Afrika (AFRAA) limejiimarisha
kama moja kati ya mashirika makubwa katika ukanda. Ushirikiano na Air
Tanzania utawapatia wateja wa Interair, njia mpya bora ya kusafiri
kwenda Tanzania na kutoka Tanzania, Johannesburg inakuwa karibu zaidi na
ni ya rahisi kufika kwa wateja wa Air Tanzania,” alisema.
Alisema
Interair ya Afrika ya Kusini ambayo ina makao yake makuu Johannesburg,
Afrika ya Kusini, kwa sasa ina ndege aina za Boeing 727, 737 na 767,
ambazo zinatoa huduma ndani ya Afrika na katika visiwa vya Bahari ya
Indi. Alikuwa
na matarajio kwamba ushirikiano huo utausaidia shirika lake kutengeneza
jina thabiti katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.



Post a Comment