Pages

May 29, 2014

HOTUBA YA BAJETI BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI YAKWAMA,KISA HIKI HAPA..

Arusha.
Hotuba ya Bajeti ya mwaka 2014/15 katka Bunge la Afrika Mashariki(Eala)haijasomwa kama ilivyokua imekusudiwa leo kwenye ukumbi wa Bunge jijini Arusha.

Kaimu Waziri wa Baraza la mawaziri wa Afrika Mashariki,Shem Bageine hakuweza kusoma bajeti hiyo baada ya Mbunge Peter Mathuki kutaka mwongozo wa Spika,Dk Margaret Zziwa kutaka hoja ya kumng'oa madarakani iliyokwama kikao kilichopita.

Mathuki alitaka kabla ya Hotuba ya bajeti kusomwa hoja iliyokuwepo ya kumwondoa Spika ijadiliwe kwanza kabla  hotuba kusomwa kwani ya msingi na Mahakama imetoa mwongozo wa kuwa kanuni za bunge hilo ni halali na bunge linaweza kuendelea na wajibu.

Hoja hiyo ilianzisha mabishano ya kisheria na kanuni huku Mwanasheria Mkuu wa EAC,Wilbert Kaahwa akitoa mwongozo wa kumtaka Spika kuruhusu hoja hiyo kujadiliwa huku Mbunge Fred Mbidde akipinga hoja hiyo hadi Mahakama itakapotoa uamuzi wa mwisho.

Spika Zziwa aliarisha kikao kwa dakika 10 kwaajili ya mashauriano na kikao kiliporejea aliarisha bunge hadi jumanne saa 4 asubuhi kwaajili ya hotuba ya Bajeti.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...