Pages

April 23, 2014

Rais Kikwete:Halmashauri nendeni mkajifunze Karatu

         Karatu,Arusha
Rais Jakaya Kikwete amekunwa na utendaji wa halmashauri ya wilaya ya Karatu. inayoongozwa na Chadema kwa kuweka utaratibu wa kuwasomesha watoto wote wenye uwezo kielimu bila kujali uwezo wa kiuchumi wa wazazi au walezi wao.
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika moja ya ziara zake za kikazi nchini.Picha na Maktaba.Kikwete aliyetembelea Karatu Aprili 22, mwaka huu pia alipongeza juhudi za uongozi wa halmashauri hiyo kutatua kero ya maji na kuahidi kuwa serikali
itamalizia fedha zinazohitaji kukamilisha mradi wa maji aliyouzindua kwenye ziara hiyo.
Halmashauri ya Karatu inaongozwa na Chadema tangu mwaka 2000 huku CCM ambayo Kikwete ni Mwenyekiti wake wa Taifa ikiwa chama pinzani. Chadema inaongoza jumla ya kata 10 huku CCM ikiwa na kata nne pekee Karatu. Chadema pia kinashikilia kiti cha ubunge Karatu tangu mwaka 1995 kupitia kwa Dk Wilbrod Slaa na sasa Mchungaji Israel Natse.
Hatua ya Rais Kikwete kusifia uongozi wa halmashauri ya Karatu chini ya Chadema kimepongezwa na wananchi, Joco Akwaso akisema kinastahili kuigwa na
viongozi wengine kwa kuweka pembeni itikadi za kisiasa kwenye masuala ya msingi ya maendeleo."Halmashauri zingine ziende Karatu kujifunza namna ya kuendeleza miji yao na kuleta maendeleo katika maeneo yao kama Karatu wameweza huko kwingine mnashindwa nini?"alisema Rais Kikwete na Kuhoji.Chanzo www.habarimpya.com

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...