Pages

April 16, 2014

NAIBU MEYA ARUSHA APEWA KICHAPO NA MGAMBO



Msofe na Nanyaro
Naibu Meya wa Jiji la Arusha, Prosper Msofe (kushoto) ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Daraja Mbili kupitia CHADEMA na Diwani wa Kata ya Levolosi, Ephata Nanyaro nae kupitia Chadema, wakisubiri kupata matibabu baada ya kupata kipigo kutoka kwa mgambo wa Jiji la Arusha leo wakati wakiwatetea Wamachinga.Kwa mujibu wa Diwani Nanyaro, anasimulia kwamba leo asubuhi alipata taarifa kuwa mgambo wa Jiji wanawapiga wananchi wafanyabiashara ndogondogo na kupora mali zao maeneo ya Kata yake, ndipo akaelekea kukutana na Naibu Meya kujionea hali halisi. Anasema alipofika alijaribu kuwasihi mgambo hao kuwa sio utaratibu kuwapiga wananchi maana hata taratibu za ukamataji haziruhusu kupiga raia.

Nanyaro anasema wakiwa wanawashauri mgambo hao, ghafla walishangaa na yeye amezingirwa na kuanza kupigwa sambamba na Msofe huku mgambo hao wakiwaeleza Madiwani hao kuwa wamekuwa na kiherehere sana.
Naibu Meya anenaAkizungumza na Blog hii Mh. Naibu Meya Prosper Msoffe ameeleza kiini cha tatizo kuwa yeye kama kiongozi wa wananchi amekuwa akipokea malalamiko mengi ya wananchi kupigwa, wengine kuvunjwa miguu, mali kuporwa na mgambo, mali kifadhiwa depoti hadi kuoza. Hivyo akaamua kufika eneo la depoti leo kujionea hali halisi na kuzungumza na mgambo na wananchi, baada ya kufika eneo la tukio alianza kushambuliwa kwa virungu na mateke, huku wakisema wewe umekuwa kiherehere sana na mtetezi wa wananchi sasa tunakukomesha. 
Mh. Naibu Meya alishangazwa pia kuona kiongozi mwenzake Diwani wa Levolosi kufika pale nae akapigwa, na kuhoji kama yeye Naibu Meya amepigwa, hali ikoje kwa wananchi wa kawaida!??
Hatua za kisheria dhidi ya mgambo hao
Hadi tunaandika taarifa hii, Madiwani hao walikuwa wanaandaa utaratibu wa kushughulikia swala hilo wakidai kwamba mgambo hao wameonesha utovu mkubwa wa nidhamu na ukiukwaji wa sheria kwa kuwapiga waajiri wao.  Msofe na Nayaro wamelaani vikali tukio hilo na kuahidi kufuatilia ili sheria ichukue mkondo wake na iwe fundisho wa wengine.
2
Kadi ya matibabu ya Kituo cha Afya Levolosi, ikionyesha Mh. Naibu Meya ALIVYOUMIZWA
5 (2)
Wananchi na Wanachama wa Chadema Wakiwa nje ya Geti la depoti ya Jiji na Kituo cha Afya cha Levolosi wakisubiri hatma ya Viongozi wao.
4
1b
Diwani Nanyaro na Naibu Meya Msofe wakimweleza Mwandishi Filbert Rweyemamu hali ilivyokuwa hadi kupigwa kwa kile walichodai kutetea wananchi wanyonge dhidi ya uonevu, ukatili na ukandamizaji unaofanywa na askari wa Jiji.
11
‘Siamini kama Wafanyakazi wangu wanaweza nishambulia kiasi hiki’ Maneno ya Nanyaro akikagua ripoti ya dakatari
IMGP1057
Mh Kessy,  Diwani wa Kaloleni (anayeongea na simu) alipofika Hospitalini hapo kuwajulia hali viongozi wenzake.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...