April 10, 2014
KAMATI ZAWASILISHA MAONI YAO UCHAMBUZI WA SURA YA KWANZA NA YA SITA YA KATIBA MPYA DODOMA.
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samuel Sitta akitoa ufafanuzi kwa wajumbe wa Bunge hilo leo mjini Dodoma wakati wa uwasilishaji wa Sura ya Kwanza na Sita wa rasimu ya Katiba mpya.
Mwenyekiti wa Kamati namba mbili (2) Shamsi Vuai Nahodha akiwasilisha maoni ya wajumbe wa Kamati yake leo mjini Dodoma juu ya uchambuzi wa sura ya kwanza na sita ya wa rasimu ya Katiba mpya.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati namba tano Assumpter Mshama akiwasilisha maoni ya wajumbe wa Kamati yake leo mjini Dodoma juu ya uchambuzi wa sura ya kwanza na sita ya wa rasimu ya Katiba mpya.
Baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakifuatilia uwasilishaji wa maoni ya wanakamati mbalimbali upande wa Sura ya kwanza na sita wa rasimu ya Katiba mpya leo mjini Dodoma.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Pandu Ameir Kificho (kushoto) na Balozi Seif Ali Idd(kulia) wakijadiliana jambo leo mjini Dodoma wakati wa uwasilishaji wa sura ya kwanza na sita wa rasimu ya Katiba mpya unaofanywa na Kamati mbalimbali.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba January Makamba (kushoto) na Dkt. Asha Rose Migiro (kulia) wakijadiliana jambo leo mjini Dodoma wakati wa uwasilishaji wa sura ya kwanza na sita wa rasimu ya Katiba mpya unaofanywa na Kamati mbalimbali.
Baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakiwasili leo kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma kwa ajili ya kusilikiliza uwasilishaji wa sura ya kwanza na sita ya rasimu ya Katiba mpya.(Picha na Bunge Maalum la Katiba).
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment