NI PINTO TENA MWENYEKITI TASWA, MPINZANI AINGIA MITINI, MHANDO NA GRACE HOKA WAPETA

JUMA Abbas Pinto amefanikiwa kutetea nafasi yake ya Uenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) leo baada ya mpinzani wake George John Ishabairu kujitoa katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika leo kwenye ukumbi wa NSSF Water Front, Dar es Salaam. 
George alitangaza kujitoa baada ya kufika ukumbini, akisema kwamba Mwajiri wake, Wizara ya Maji amemwambia ajitoe. 


Kamati mpya ya Taswa
Wanaume tumerudi; Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto kulia akipongezana na Katibu wake, Amir Mhando baada ya kutangazwa washindi mchana huu ukumbi wa NSSF Water Front, Dar es Salaam.


 Pinto alipata kura 82 wakati 13 zilimkataa, na Egbert Mkoko ameshinda nafasi ya Makamu Mwenyekiti kwa kura 67 dhidi ya 32 za Mohammed Omary Masenga.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Boniface Wambura Mgoyo alimtaja Amir Mhando kushinda tena nafasi ya Ukatibu Mkuu baada ya kupata kura 93. Mhando hakuwa na mpinzani na kura mbili tu zilimkataa.
Nafasi ya Katibu Msaidizi imekwenda kwa Grace Aloyce Hoka aliyepata kura 65 dhidi ya 31 za Alfred Lucas Mapunda.
Aliyeshindwa; Elizabeth Mayemba kulia aligombea Ujumbe akashindwa. Mwani Nyangassa wa pili ameshinda na kushoto ni mpiga kura Zaituni Kibwana


Sophia Asheri kulia na Somoe Ng'itu kushoto
Mhariri wa magazeti ya mwishoni mwa wiki ya Habari Leo, Eric Anthony Mkuti kulia


Lehule Nyaulawa kulia akipongezana na Grace Hoka


Post a Comment

Previous Post Next Post