Katibu
Tawala Mkoa wa Katavi akimwongoza Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya
Jamii,Jinsia na Watoto, Anna Maembe wakati akikagua eneo la chuo cha
maendeleo Msaginya wakati wa ziara yake ya siku mbili mkoani humo anaye
mfuatia kushoto kwa Katibu Mkuu ni Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri
ya Wilaya Nsimbo Alex Magesa Na Mwisho mwenye SUTI YA kijivu ni Mkuu wa
Chuo Msaginya Peter Kikunda ambaye ni mwenyeji akiwatembeza wageni.
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto, Anne Maembe akipatiwa
maelezo kuhusu bweni la wananchi wa kike liliezuliwa na upepo kufuatia
mvua mwaka jana hali iliyofanya kusimama kwa masomo katika chuo hicho
kutokana na ukosefu wa mahali pa kulala kwa wanafunzi wa kike.
Baadhi
ya majengo ya chuo Msaginya yanaonekana kuchaka kutokana na kukosa
ukarabati kwa muda mrefu hali inayoonesha chuo kama vile kimesahaulika
ambacho kinamilikiwa na wizara ya maendeleo ya jamii,lakini ni mali ya
wananchi ingawa hawaoni umuhimu wa kuwa na chuo hicho,juhudi za makusudi
zinahitajika na ubunifu zaidi ili kunusuru chuo hicho.
Na Kibada Ernest- Katavi.
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto,Anna
Maembe ameshauri watendaji wa Wizara hiyo kuwa wabunifu katika utendaji
wao wa kazi za kila siku kwenye maeneo yao ili kuleta mabadiliko katika
jamii wanayoitumikia katika utendaji wao wa kazi.
Katibu
Mkuu alitoa kauli hiyo mkoani Katavi alipokutembelea mkoa huo na
kukutana na watendaji wa Wizara yake na kupata nafasi ya kukitembelea
Chuo cha Maendeleo ya wananchi Msaginya kilichoko Halmashauri ya Nsimbo
Wilayani Mlele ambacho kinakabiliwa na changamoto kibao hali
iliyosababisha kushindwa kusajiri wanachuo wa kujiunga katika fani
mbalmbali mwaka huu wa masomo.
Mbali
ya kukitembelea Chuo hicho pia alipata nafasi ya kukutana na vikundi vya
vya kinamama waliojiunga pamoja kw a ajili ya kupata na mikopo
wanayowezeshwa na Halmashauri kutokana na fedha za ndani ili kuwajengea
uwezo akimama waweze kuondokana na utegemezi kwa kuanzisha baiashara
ndogondogo ambazo huwasaidia kujikimu kimaisha katika familia zao kama
kusomesha watoto,matibabu na huduma nyingine za kijamii.
Pamoja
na kukutana na vikundi vya uzalishaji mali kutoka kwenye Halmashauri za
Mkoa huo za Wilaya Mpanda,Halmashauri ya Nsimbo,pamoja na ile ya Mji wa
Mpanda kupokea changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo akinamama
hao, pia alipata nafasi ya kukutana wakurugenzi wa Halmashauri hizo na
wakuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii pamoja na wafanyakazi wa Idara hizo
akapokea changamoto zinazowakabili katika utendaji kazi na namna ya
kukabiliana nazo.
Awali akiwa katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi alipokea Taarifa ya Mkoa kuhusu utekelezaji wa kazi za Idara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto iliyotolewa
na Katibu Tawala wa Mkoa Mhandisi Emmanuel Kalobelo kwa kueleza namna
Mkoa ulivyojpanga kukabiliana na changamoto zilizopo najinsi
wanavyosaidia kuwawezesha wananachi kuondokana na umasikini hasa kupitia
Halmashauri zimejipanga kuwezesha kwa kuunda vikundi vya akinamama
pamoja na vijana kuwawezesha kujiaajili kwa kutumia rasilimali zilizoko
kwenye maeneo yao.
Akiongea
katika kikao hicho Mhandisi Kalobelo alimweleza jinsi Mkoa kupitia
kwenye Halmashauri zinavyotekeleza utendaji kazi kwa kuwaunganisha
wananchi ili kuwaletea maendeleo,kwa kuanzisha miradi ya kiuchumi
kupitia kwenye vikundi vya uzalishaji mali vya akina mama na Vijana
kujiunga pamoja na kuwezeshwa mikopo kupitia kwenye Halmashauri.
Akizungumzia
kipimo cha utendaji kazi kwa mtu kuwepo kwenye nafasi Fulani
aliyoanayoatapimwa na kwa ufanisi wake kuonekena katika nafasi hiyo
ameleta mabadiliko gani kutokana na uwepo wake pale ameisaidiaje jamii
kutokana na uwepo katika nafasi hiyo.
Alisisitiza
kuwa itafika wakati kujitathimini kwa kila mmoja nini amefanya kwa
nafasi aliyonayo katika kutekeleza majukumu yake, katika nafasi
aliyokabidhiwa katika kuleta mabadiliko yenye tija katika jamii.
Katibu
Tawala huyo alieleza kuwa ni muhimu kwa kila mmoja kuwa mbunifu na
kusoma mazingira ya eneo analofanyia kazi atumie rasilimali zilizopo
kuweza kuwanufaisha wale anaowatukia awe mbunifu kwa ajili ya maendeleo
ya eneo lake.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashuri ya Halmashauri ya Mpanda
Estominh Chang’ah alimweleza Katibu Mkuu kuwa Halmashauri ya Mpanda
iwejiwekea mikakati ya kuwaletea wananchi maendeleo kwa kupitia makundi
ya akinamama na VIjana kwa kuwahamasisha kujiunga kwenye vikundi vya
uzalishaji mali na kuwawezesha mikopo kutoka kwenye mfuko wa maendeleo
jamii kwa kutumia fedha zilizotolewa Halamashuri.
Akizungumzia
suala la kukopa amesema menejementi ya ukopaji ya mikopo bado
haijaingia ipasavyo miongoni mwa jamii,na mtu akipewa mkopo bado
urejeshwaji wake bado uko chini, Halamashauri katika kukabiliana na
changamoto hizo imejipanga na kujiwekea mikakati mizuri kuwahamasisha
wakopaji kwa kuwape elimu namna ya kurejesha ili wengine waweze kukopa
kwa kuwa fedha hizo zinatakiwa ziwafikie wote.
Katika
kukabiliana na utatuzi wa changamoto za uhaba wa fedha Halmashauri
imeingia mkataba na benki ya TID ili iweze kuwa inakopesha wajasiliamali
wilayani mpanda ili kuondoa tatizo la ukosefu wa fedha, Mkakati
mwingine ni Halmashauri kukikwezesha kiwanda cha uzalishaji mafuta cha
Mpadeco, kuweza kusaidia kupatiwa malighafi kwa kutumia mashamba ya
alizeti ili kutoa malighafi kwa ajili kuzalisha mafuta kwenye kiwanda
hicho na ili waweze kuunza mafuta badala ya alizeti na kuongeza thamani
ya mazao.




Post a Comment