KAMPUNI YA MONABAN YAKABIDHI MSAADA HAI KWAAJILI YA WAANGA WA MAAFA

DSCF2880Mkurugenzi wa kiwanda cha kuzalisha unga kilichopo jijini Arusha Bw.Philemon Mollel akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Hai Mh.Novatus Makunga msaada wa Tani nne za unga  wenye thamani ya shilingi Milioni 4.2,baada ya wilaya yake kupata maafa yaliyotokana na mvu zilizoambatana na upepo mkali na kusababisha badhii ya watu kukosa nyumba za kuishi
DSCF2878Mkurugenzi wa kiwanda cha kuzalisha unga Arusha Philemon Mollel akiongea mbele ya wanakijiji(hawapo pichani)namna alivyoguswa na maafa hayo yaliyopelekea kutoa msaada huo huku kiwataka wafanyabishara,makampuni,watu binafsi kujitokeza kuwasaidia waanga wa maafa hao,mbali na msaada huo wa tani nne za unga pia alitoa shilingi Milioni moja kwaajili ya waanga
DSCF2861 
DSCF2857Mkuu wa wilaya ya Hai Mh.Novatus Makunga akiwa na ugeni mzito kutoka kampuni ya Monaban ofisini kwake,lengo la ugeni huo nikutoa msaada wa chakula kwa waathirika wa maafa ya mvua

DSCF2866Kina mama ambao ndio waathirika wa kubwa wa maafa hayo wakisubiria zoezi la kugawiwa chakula cha msaada
DSCF2870Mtendaji wa kijiji Bi.Trea Ramadhani akitoa shukrani zake za dhati kwa mmiliki wa kiwanda cha kuzalisha unga kilichipo Arusha

DSCF2874Wanakijiji wakishuhudia msaada ulioletwa kijijini kwao
DSCF2882Mkuu wa wilaya Novatus Makunga akimkabidhi msaada uliotolewa na kampuni ya Monaban ,mtendaji wa kijiji cha  kwa sadala Bi.Trea Ramadhani msaada uliogharimu zaidi ya milioni 4,Kushoto ni kaimu mkurugenzi Bw.Zabdieli Moshi
DSCF2883Mkuu wa wilaya ya Hai Mh.Novatus Makunga akitoa shukrani zake za dhati kwa mmiliki wa kiwanda cha Monaban kwa kuweza kuwaletea chakula cha msaada na kuwataka makampuni,mashirika na watu binafsi kuiga mfano wa Monaban kwa kuwasaidia waanga wa maafa yaliyotokana na mvua zilizoambatana na upepo mkali na kusababisha watu kukosa makazi hivi karibuni ktika wilaya yake



Nyumba ya familia ya Bibi Aziza Mohammed baada ya kuezuliwa paa
Bibi Aziza Mohammed kama anavyooneka katika picha baada ya mvua kusababisha mafaa makubwa kwake hali iliyosababisha yeye kuishi chooni na mjuuku wake
(Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)

Post a Comment

أحدث أقدم