CCM YASISITIZA MSIMAMO WAKE WA SERIKALI MBILI, NEC YATOKA NA MAPENDEKEZO YA MABORESHO YA SERIKALI HIZO


Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesisitiza msimamo wake katika Katiba mpya kuwa ni wa serikali mbili.

Lakini kimesema licha ya msimamo wake kuwa huo kinataka serikali mbili zilizofanyiwa maboresho kuondoa kero za 
Muungano zilizopo ambazo imesema kwa vyovyote vile haziwezi kuondolewa kwa mfumo wa serikali tatu.

Hayo yamesemwa leo na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizungumza yaliyojiri katika Kikao cha siku mbili cha Halmashauri Kuu ya CCM, kilichomalizika jana  Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma.

Nape amsema kikao hicho kilichokuwa chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, kimezichambua kwa moja baada ya nyingine, kero za muungano na Chama kitaziwasilisha kwenye bunge la Katiba kama msimamo wake.

Akizungumzia kauli ya wapinzani hususan Chadema kutangaza kwamba CCM huenda italiburuza bunge la Katiba kutokana na wingi wa wabunge ilio nao.
 Nape alisema, huo ni wasiwasi tu, na kwamba kama wanataka kwenda kwa
wananchi watangulie mapema na CCM pia itakwenda kwa wananchi hao hao kuwapa majibu. 
Pichani Nape akizungumza na Waandishi wa Habari leo nje ya jengo la White House la Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma

Post a Comment

أحدث أقدم