Taarifa za uhakika kutoka mjini Mugumu Wilayani Serengeti
zinapasha kuwa diwani wa kata ya Stendi Kuu Mwalimu MARWA RYOBA (CHADEMA) ameswekwa ndani kwa amri ya mkuu wa
wilaya.
Kadhia hiyo imemkumba diwani huyo ambaye pia ni maarufu sana
mjini Mugumu kwa juhudi zake na ujasiri wake wa kutetea maslahi ya wananchi wa
kata yake, wananchi wa mamlaka ya mji mdogo wa Mugumu pamoja na wilaya ya
Serengeti kwa ujumla. Diwani huyo ambaye ni Katibu Mwenezi wa Chadema Wilaya ya
Serengeti pia ametangaza nia ya kugombea ubunge mwaka 2015 na amekuwa akifanya
mikutano maeneo mbalimbali wilayani humo akihimiza ujenzio na uimarishaji wa
Chadema.
Baada ya kumalizika kwa vikao vya baraza la madiwani wilaya ya
Serengeti Diwani Mwalimu Ryoba aliona ni busara kufanya mrejesho kwa wapiga kura
wake juu ya mipango ya halmashauri kuhusu kata yao.
Katika mikutano hiyo
iliyofanyika katika vitongoji vya Kyabakari,Chamoto na Bomani, diwani alikuwa
akisikiliza na kupokea kero mbalimbali za wananchi. Mojawapo ya kero kubwa
ambayo wananchi waliilalamikia ni zoezi la ukamataji wa mifugo hasa ng'ombe,
zoezi linaloendeshwa na migambo wa mamlaka ya mji mdogo wa Mugumu. Niwafahamishe
tu kwamba mamlaka ya mji mdogo Mugumu ndiyo yameanzishwa hivi karibuni na
vitongoji vilivyomo katika kata ya Stendi kuu inayounda sehemu ya mji mdogo wa
Mugumu wakazi wake wengi takribani 95% ni wafugaji.
Katika malalmiko hayo
ya wananchi wakabainisha kuwa migambo hao wamekuwa wakivizia mifugo katika
maeneo yasiyozuiliwa na kuwakamata kasha mtendaji wa kata anawatoza faini, Jambo
la ajabu ni kwamba mtendaji huyo amekuwa akiwapatia risiti za bandia ambazo
hazina alama yoyote ya kuthibitisha kuwa ni risiti halali (nimeweka
kiambatanisho).
Baada ya kusikiliza kero hiyo diwani Ryoba aliwataka
wananchi wampe taarifa mara tu migambo watakapokamata mifugo yao na kuahidi kuwa
suala hilo angelifuatilia kwa mtendaji wa kata na Mkurugenzi wa halmashauri.
Alipokwenda kumhoji mtendaji na kumtaka aeleze ni kwanini anawakatia wananchi
risiti feki ndipo zengwe lilipoanzia kwa mtenadji huyo kupeleka malalamiko kwa
mkurugenzi kuwa diwani amemzuia kufanya kazi yake.
Siku mbili baadae
Polisi wa kituo kikuu cha Mugumu mjini walimpigia simu diwani wakimtaka afike
kituoni hapo. Diwani aliitikia wito na kufika polisi Mugumu kama alivyoitwa na
alipofika kwa OCS akawekwa chini ya ulinzi na kufunguliwa mashitaka ya uchochezi
na kutishia uvunjifu wa amani.
Baada ya kufikishwa mahakamani tarehe
20/01/2014 na kusomewa mashitaka yake ya uchochezi na kutishia uvunjifu wa
amani, polisi waliweka pingamizi la mshitakiwa kutopewa dhamana kwa madai kuwa
kama akipewa dhamana ataingilia upelelezi na kwamba mtuhumiwa mwingine mmoja
alikuwa bado hajakamatwa, na hivyo basi kesi imeahirishwa hadi tarehe 03/02/2014
itakapotajwa tena.
Baada ya makamanda kufuatilia kwa undani toka chanzo
cha uhakika kutoka polisi Mugumu imebainika kuwa Diwani mwalimu Ryoba amekamatwa
kwa amri ya mkuu wa wilaya ikiwa ni njia ya kumkwamisha kisiasa kwakuwa diwani
huyo anatishia kabisa nafasi ya ccm kushinda Ubunge Serengeti na hata kuongoza
halmashauri ya wilaya na mamlaka ya mji mdogo wa Mugumu.
Kwa wale waliopo
Mugumu wanaweza kumtembelea kamanda Ryoba katika mahabusu ya Mugumu Mjini
iliyopo karibu kabisa na hospitali teule ya wilaya, Mugumu DDH.Chanzo JF
Post a Comment