Habari zinasambaa kuhusu ndege kubwa ya shirika la Ethiopian Airlines ikiwa na abiria zaidi ya 300 imetua kwenye majani wakati ikijaribu kutua kwa dharura katika uwanja mdogo wa ndege wa Arusha Airport, mkoani Arusha.
Ndege hiyo imetua katika uwanja huo unaotumika na ndege ndogo tu, baada ya kushindwa kutua uwanja wa ndege wa KIA, kufuatia kuwepo ndege iliyoharibika kwenye njia ya uwanja huo.
Hii hapa ni picha ya ndege hiyo ilivyotua na kusimama kwenye majani.
Ukubwa wa ndege hii inaripotiwa kwamba ni kubwa sana kutua kwenye uwanja wa Arusha ndiyo maana hadi kusimama imesimama kwenye majani ambapo ni nje ya uwanja





إرسال تعليق