Pages

December 8, 2013

KWAYA YA UINJILISTI KIJITONYAMA KUFANYA TAMASHA LA KUADHIMISHA JUBLEI YA MIAKA 25 JUMAPILI HII

Kwaya ya Kijitonyama Uinjilisti jijini Dar es Salaam watarajia kufanya tamasha la kusherekea jubilee ya miaka 25 ya kwaya ya yao. Tamasha hilo la aina yake linatarajiwa kufanyika Jumapili ya tarehe 8/12/2013 Kanisani hapo kuanzia saa 7 mchana hadi saa 12 jioni. Kwa mujibu wa Meneja Mipango wa Kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama, Onai Joseph amesema kuwa wamewaalika Kwaya ya Tumain St. James kutoka Arusha na Kwaya zote za K.K.K.T Kijitonyama. Hakuna kiingilio ni BUREE!!
Viongozi wa kwaya ya Kijitonyama wakiongea mbele ya waandishi wa habari.
Mwimbaji Modesti Mogani, Mwimbaji na Mtunzi Oliver Israel anasema kuwa siku ya tamsaha kutauzwa CD na DVD ya albamu zao zote za zamani ikiwemo mpya iliyozinduliwa hivi karibuni ya 'Namtangaza Kristo'.
Wanakwaya wa Kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama wakitoa burudani mbele ya waandishi wa habari.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...