Katibu
Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad amesema
chama chake kitaendelea kusimamia misingi ya haki na usawa, ili
kuhakikisha kuwa kila Mzanzibari anapata haki yake inayostahiki.
Maalim
Seif ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ameeleza hayo
wakati akihutubia mkutano wa hadhara ya chama hicho uliofanyika viwanja
vya Kinyasini, jimbo la Chaani.
Amesema
Chama hicho kitaendelea kuwa mstari wa mbele kudai mamlaka kamili ya
Zanzibar kwa lengo la kuhakikisha kuwa Zanzibar inaongozwa kwa misingi
ya haki na usawa, ili wazanzibari waweze kuamua mambo yao wenyewe bila
ya kuingiwa na mamlaka nyengine.
Amesifu
umakini wa kamati ya Maridhiano yenye wajumbe sita wakiwemo watatu
kutoka Chama Cha Mapinduzi na watatu kutoka Chama Cha CUF, na kwamba
wajumbe wa kamati hiyo wameonesha uzalendo wa hali ya juu katika
kutekeleza majukumu yao.


إرسال تعليق