Balozi Seif akiwa pembezoni mwa dirisha ndani ya chumba cha chini ya Bahari akiangalia samaki na mazingira yake mara baada ya kuuzindua mradi huo hapo Manta Resort Hoteli Makangale.
Balozi
Seif akiangalia ngazi ya kutokea juu ya chumba cha chini ya Bahari
katika Hoteli ya Manta Resort Makangale Mkoa wa Kaskazini Pemba kwenye
sherehe za uzinduzi wa chumba hicho ikiwa ni
muendelezo wa sherehe za kutimia miaka 50 ya mapinduzi ya Zanzibar
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akimpongeza Meneja
Mkuu wa Hoteli ya Manta Resort Bwana Methew Saus kwa kukamilisha
ujenzi wa chumba cha chini ya Bahari kwenye hoteli yake iliyopo
Makangale Mkoa wa Kaskazini Pemba huku Waziri wa Habari Mh.
Marouk akifurahia kitendo hicho.
Kitanda na mandhari halisi na nzuri iliyomo ndani ya chumba cha chini ya Bahari katika hoteli ya
Manta Resort Makangale Kaskazini Pemba mradi uliozinduliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar balozi Seif.
Sehemu ya choo katika chumba cha chini ya Bahari kilichopo kwenye Hoteli ya Manta Resort huko Makangale Pemba.
Meneja Mkuu wa Hoteli ya Manta Resort Bwana Methew Saus Maarufu
“ Babu kwa Nini “akitoa maelezo ya hatua zilizochukuliwa kukamilisha
ujenzi wa chumba cha chini ya Bahari katika Hoteli ya Manta Resort
iliyoko Makangale Mkoa wa Kaskazini Pemba.Kushoto ya Balozi
Seif ni Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi, Waziri wa Habari, Utamaduni,
Utalii na Michezo Mh. Said Ali Mbarouk na Naibu wake Mh. Bihindi Hamad.
Meneja Mkuu wa Hoteli ya Manta Resort Bwana Methew Saus akionyesha
eneo la juu la chumba cha chini ya bahari ambapo mgeni atapata fursa ya kupunga upepo pamoja na kuota jua.
Mandhari nzuri ya Hoteli ya Manta Resort ya Makangale Mkoa wa
Kaskazini Pemba eneo ambalo kipo chumba cha chini ya Bahari.
Na Othman Khamis Ame Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Mradi mpya wa ujenzi wa Chumba cha chini ya Bahari uliofanywa na Hoteli ya Manta Resort iliyopo katika Kijiji cha Makangale Mkoa wa Kaskazini Pemba umeiweka Zanzibar katika ramani mpya ya Dunia katika harakati za kuimarisha sekta ya Utalii unaobeba nafasi kubwa ya Uchumi katika
Chumba hicho cha chini ya Bahari kilichopo Makangale ambacho ni cha
pekee Barani Afrika kimeiwezesha Zanzibar kuwa ya tatu kwa kuwa na
mradi kama huo Duniani ikitanguliwa na Nchi za Puerto Riko,Sweden,
Kisiwa cha Fiji na ikifuatiwa na Dubai.
Mradi huo ulioko katika Matengenezo unatarajiwa kuwa na vyumba
takriban
220. Jengo hilo lenye huduma kamili anazostahiki kuzipata mwanadamu ni
pamoja na chumba cha kulala,huduma za maji safi,Choo, umeme, sehemu ya
Mapumziko, na eneo maalum la juu kwa ajili ya kuotea
jua.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ambae ndiye
aliyeweka Nanga ya Msingi ya mradi huo wa Makangale Miezi 12 iliyopita
Tarehe 25/12/2012 akakizindua tena rasmi chumba cha mradi huo
kilichoko umbali wa mita Nne chini ya Bahari.
Uzinduzi huo uliojumuisha mamia ya Wananchi wa Kijiji cha Makangale
pamoja
na majirani zake ulishuhudiwa pia na Viongozi kadhaa wa Serikali, vyama
vya Siasa pamoja na watendaji wa Sekta ya Utalii wakiongozwa
na Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Mh. Said Ali Mbarouk
na Naibu wake Mh. Bihidndi Hamad.
Akizungumza mara baada ya kuuzindua Mradi huo Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Balozi Seif alisema kwamba uwepo wa mradi huo wa
chumba cha chini ya Bahari ni kielelezo muhimu kitakachokuwa kivutio
kwa wageni katika harakati za kukuza utalii hapa Zanzibar.
Balozi Seif aliupongeza Uongozi wa Hoteli ya Manta Resort ya Makangale
kwa
kuamua kuwekeza mradi huo wa kipekee Barani Afrika ambao utaleta
maendeleo makubwa katika Sekta ya Utalii. “ Nimeshuhudia uzuri wa
chumba hichi ambapo yapo mazingira mazuri ya mapumziko na kulala,
samaki wa kuvutia.
Natarajia wakaazi wanaonguuka eneo hilo watashirikiana vyema na
uongozi wa
Hoteli hiyo katika kukilinda chumba hicho kinachotarajiwa kuongeza
ushawishi kwa watalii kutembelea Zanzibar “. Alisisitiza Balozi
Seif.
Alielezea
matumaini yake kwamba Uongozi wa Hoteli ya Manta Resort Makangale
utaendelea kutoa huduma bora na za uhakika ili kuongeza idadi ya wageni
na watalii kutembelea Pemba. Katika kuunga mkono jitihada hizo za
wawekezaji alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuwapa
mashirikiano ya karibu wawekezaji wa sekta hiyo ili waendeshe shughuli
zao kwa ufanisi mkubwa.
“
Sisi Viongozi wa Serikali akiwemo Mheshimiwa Rais, Makamu wa Kwanza wa
Rais na mimi mwenyewe tunapofanya ziara nje ya nchi hutumia fursa ya
kuwabembeleza wawekezaji kuwa kuwekeza Nchini mwetu hasa katika sekta ya
utalii na Viwanda.
Bahati
nzuri wanatuitikia na wanakuja na ndio maana leo Zanzibar ina vitega
uchumi vingi vya sekta ya utalii na mfano hai ni huu mradi wa chumba cha
chini ya Bahari hapa Makangale “. Alifafanua Balozi Seif.
Alifahamisha
kwamba pamoja na maendeleo ya ujenzi wa miradi ya uwekezaji katika
sekta ya utalii lakini bado Serikali pamoja na Wananchi wanahitaji
kuendelea kuwa na matumaini ya kuongezeka kwa idadi ya watalii hali
ambayo itasaidia kuongeza mapato ya Taifa.
Hata
hivyo Balozi Seif alitahadharisha kwamba watalii na wageni hao
hawataingia nchini iwapo jamii haitojikita katika kuendeleza amani na
utulivu ndani ya maeneo yao hasa sehemu zenye vitega uchumi hivyo.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema wananchi hawanabudi kupania kuiweka
nchi katika hali hiyo ya amani na usalama ili wageni hao washawishike
kupenda kuendelea kutembelea Nchini na kuishi bila ya wasi wasi.
“
Tuwe wanyenyekevu kwa wageni wetu, tuwaonyeshe bashasha za Kizanzibari
kama ilivyo tabia na desturi yetu, tusiwabughudhi wakiwa ufukweni au
katika matembezi yao. Tunataka wafurahie ukaazi wao katika visiwa vyetu
vya karafuu na Viungo “. Alieleza Balozi Seif.
Mapema
Meneja Mkuu wa Hoteli ya Manta Resort Bwana Methew Saus Maarufu “ Babu
kwa Nini “ alisema utafiti wa mradi huo ulifanyika kwa karibu miaka sita
ambapo wataalamu wa kimazingira na mambo ya bahari walilazimika kupima
mwenendo wa maji ya bahari ya eneo hilo ili kuwa na uhaika wa kuanzisha
mradi huo.
Bwana
Methew Saus alisema mazingira ya Kisiwa cha Pemba yamepelekea
kuanzishwa kwa mradi huo wa majaribio wa chumna cha chini ya Bahari
uliogharimu zaidi ya Dola za Kimarekani Laki Tano { U$ 500,000 } sawa na
fedha za Kitanzania Milioni Mia 758,000,000/-.
Meneja
huyo wa Hoteli ya Manta Resort ya Makangale ameipongeza Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Wizara inayosimamia Sekta ya Utalii kwa
ushirikiano iliyompa kuweza kufanikisha mradi huo muhimu kwa maendeleo
ya uchumi wa Zanzibar.
Akimkaribisha
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Waziri wa Habari,
Utamaduni, Utalii na Michezo Mh. Said Ali Mbarouk alisema mradi huo kwa
kiasi kikubwa umeanza kuitangaza vyema Zanzibar katika sekta ya utalii
wa Daraja la juu duniani.
Waziri
Mbarouk aliwaasa wananchi na hasa wavuvi wanayoizunguuka hoteli hiyo
kujiepusha na uvuvi pembezoni mwa mradi huo jambo ambalo litaondoa sifa
na mazingira halisi ya kuwepo kwa samaki wanaokizunguuka chumba hicho.
Alikemea
tabia iliyoanza kujichomoza ya baadhi ya wavuvi wa maeneo hayo ya kuvua
kwa kutumia nyavu ndogo nje ya chumba hicho kwani inaweza kumvunja moyo
muwekezaji huyo ambae ameshajitolea kusaidia maendeleo ya Vijiji jirani
na Hoteli hiyo.
Mradi
wa mwanzo wa ujenzi wa vyumba vya chini ya Maji Jules Undersea Lodge
umeanza Nchini Puerto Rica mwaka 1970, Utter In Vasteras Sweden Mwaka
2000, Poseidon Undersea Resort Fiji na Mwengine Crescent Hydropolis
unaendelea kujengwa Nchini Dubai.
No comments:
Post a Comment