WAZIRI KAWAMBWA AKIMWAGIA SIFA CHUO CHA UFUNDI ARUSHA
rweyemamuinfo.blogspot.com0
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Dk Shukuru Kawambwa akipata maelezo ya Uchongaji na kung'arisha madini ya Vito kwenye banda la Chuo cha Ufundi Arusha(ATC)kwenye maonesho ya Madini yaliyofungwa jana jijini Arusha.Chuo hicho ndio pekee cha umma kinachotoa mafunzo hayo kwa ngazi ya Cheti.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Dk Shukuru Kawambwa(kushoto) akipata maelezo ya Uchongaji na kung'arisha madini ya Vito kutoka kwa mwanafunzi John Jeremia kwenye banda la Chuo cha Ufundi Arusha(ATC)Chuo hicho ndio pekee cha umma kinachotoa mafunzo hayo kwa ngazi ya Cheti.
Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha(ATC)Dk Richard Massika akifafanua jambo kwa waandishi wa habari.
Waziri wa Elimu,Dk. Shukuru Kawambwa(kulia)akipokea zawadi ya Kito kutoka kwa Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha(ATC)Dk. Richard Massika alipotembelea banda lao ili kuhamasisha wanafunzi kujiunga na Chuo hicho kujifunza Uchongaji na kung'arisha madini ya Vito .Chuo hicho ndio pekee cha umma kinachotoa mafunzo hayo kwa ngazi ya Cheti.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Dk Shukuru Kawambwa amekipongeza Chuo cha Ufundi Arusha(ATC) kwa ubunifu wa kuanzisha Kozi ya Uchongaji Madini hatua itakayoongeza thamani ya madini yanayouzwa nje na kuwapa vijana ajira.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Dk Shukuru Kawambwa(kushoto),Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha(ATC)Dk.Richard Massika na Mwandishi Mkongwe wa The Citizen wakibadilishina mawazo jana baada ya kutembelea baada la Chuo hicho na kuwapongeza kwa ubunifu wa kuanzisha Kozi ya Uchongaji Madini hatua itakayoongeza thamani ya madini yanayouzwa nje na kuwapa vijana ajira.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Dk Shukuru Kawambwa(wa tatu kulia),Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha(ATC)Dk.Richard Massika(kulia)Mratibu wa Lapidary&Jewellry,Shahzmin Premji na kushoto ni Afisa Uhusiano Mwandamizi wa ATC,Gasto Leseiyo.
Post a Comment