Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC)anayeshughulikia Miundombinu,Dk Enos Bukuku akizungumza na waandishi wa habari jijini Kampala leo juu ya hatua zilizofikiwa katika kuweka saini Itifaki ya Sarafu Moja jumamosi wiki kwenye Uwanja wa Kololo nchini Uganda,kushoto ni Mkufunzi na Mwandishi Mkongwe,Jenerali Ulimwengu.
Na Mwandishi Wetu,Kampala
Wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC)jumamosi wiki wanaweka saini Itifaki ya Sarafi Moja ikayowezesha matumizi ya Sarafu moja katika nchi hizo.
Matumizi ya Sarafu moja yatachukua muda kutekelezwa ili kutoa nafasi ya utekelezaji wa michakato mbalimbali ya kuoainisha sera na sheria ikiwa ni pamoja na kuanzishwa kwa taasisi kadhaa kabla ya kuanza kutumika Sarafu hiyo inaweza kuchukua miaka 10.
Akizungumza na waandishi wa habari leo ,Naibu Katibu Mkuu wa EAC anayehusika na Miundombinu,Dk Enos Bukuku amesema utaratibu huo utazifanya nchi wanachama kukubaliana katika mambo ya sera za fedha za Jumuiya hiyo na kuwa na Benki Kuu ya EAC.
Amesema wataalamu katika Sekretariat ya Jumuiya hiyo wamekua wakienda kujifunza mfumo wa utendaji kazi wa Sarafu moja kwenye nchi za Umoja wa Ulaya(EU). |
No comments:
Post a Comment