Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na Mbunge wa Jimbo la Peramiho Ndugu Jestina Mhagama mara baada ya kuwasili katika eneo la Seminari Kuu wilaya ya Peramiho.
Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akisalimiana na Mbunge wa Peramiho Ndugu Jenista Mhagama .
Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye mavazi ya jadi yajulikanayo kama Mgolole na kukabidhiwa silaha za jadi alipowasili katika kijiji cha Peramiho B.
Wanachama wa shina namba 28 wakishangilia hotuba ya Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye yupo kwenye ziara ya kukagua uhai wa chama katika Mkoa wa Ruvuma.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akinywa chai nyumbani kwa Balozi wa Nyumba 10 Issa Said,Katibu Mkuu amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha mabalozi wa nyumba 10 wanatembelewa na viongozi wa ngazi zote.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na viongozi na wananchi wa Peramiho wakishiriki kubeba matofali ya ujenzi wa Zahanati ya Kahegwa.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa kata ya Kahegwa baada ya kushiriki shughuli za kubeba matofali kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ya Kahegwa,Katibu Mkuu aliwaeleza wananchi hao kuimarisha moyo wa kujitegemea kwani maendeleo ya Tanzania yataletwa na Watanzania wenyewe na si wahisani.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na mmoja wa wananchi aliyefarijika sana kwa kumsikia Katibu Mkuu akizungumza maneno ya msingi na yenye kutia moyo sana hasa katika suala la kujitegemea.









Post a Comment