Na Filbert Rweyemamu,Arusha
Tanzania imepata heshima ya kuwa mwenyeji wa mkutano mkuu wa 34 wa
jukwaa la mabunge ya nchi wanachama wa jumuiya ya maendeleo ya kusini
mwa Afrika (SADC),utakaofanyika oktoba 16 mwaka huu hadi 24 ,jijini
Arusha.
Akizungumza na waandishi wa habari,spika wa bunge la jamhuri ya
muungano Tanzania ,Anne Makinda alisema kuwa,mkutano huo utatanguliwa
na vikao vya kamati mbalimbali vya jukwaa hilo, na unatarajiwa
kufunguliwa na makamu wa Rais Dkt,Gharib Bilal katika ukumbi AICC.
Alisema jukwaa hilo lililoanzishwa mwaka 1997,likiwa na malengo ya
kuimarisha utekelezaji wa uamuzi wa SADC,kwa kuimarisha wabunge katika
shughuli za SADC,kusimamia utekelezaji bora wa sera na mipango ya SADC
ikiwa ni pamoja na itifaki na mambo mengine ya kisheria.
Kusimamia misingi ya haki za binadamu ,usawa wa jinsia na demokrasia
katika kanda ya SADC,kuhakikisha uwepo wa amani,usalama na demokrasia
kwa nchi wanachama,kusimamia dhana nzima ya maisha bora ya sasa na
yajayo kwa watu wa kanda hii ili waweze kujitegemea.
Kuratibu mawasiliano na wabunge /mabunge mengine ikiwa ni pamoja na
asasi za kitaifa na mataifa,kutoa ushawishi kwa vyama visivyokuwa vya
kiserikali ,Asasi na jamii za kisomi, kushiriki kikamilifu katika
shughuli mbalimbali za SADC.
Kutoa fursa ya majadiliano juu ya mambo yanayogusa hisia za nchi
wanachama,kuhakikisha uwepo wa utawala bora ,uwazi na uwajibikaji
katika kanda hii na taasisi za SADC,kuratibu uridhiwaji na utekelezaji
sera na sheria kwa nchi wanachama ,kusimamia na kuelimisha wanachama
wa SADC kuhusu dhamira na madhumuni ya SADC na hatimaye jukwaa hili
kuwa binge la kanda ya SADC.
Aidha alisema jukwaa hilo limefanikiwa kuongeza idadi ya wanawake
kwenye mabunge ya nchi wanachama ,uangalizi wa chaguzi kwenye nchi
wanachama.
Hata hivyo alisema nchi tatu wanachama wa SADC,zimefanikiwa kufikia
asilimia 30 ya wabunge wanawake katika mabunge yake,ambazo ni pamoja
na Tanzania,Afrika Kusini na Msumbiji,lengo ni kuhakikisha wabunge
wanawake wanafikia asilimia 50.
Mkutano huo watawashirikisha wajumbe 150 wakiongozwa na
maspika,wabunge kutoka nchi wanachama wa SADC,pamoja na wadau kadhaa
kutoka taasisi mbalimbali za kimataifama,ambapo majadiliano yatajikita
zaidi kutathimini mienendo na matokeo ya chaguzi katika nchi za SADC.
Makinda alizitaja nchi zinazoshiriki mkutano huo kuwa ni Afrika
kusini,Angola,Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Congo,Lesotho,Malawi,Mauritius,Msumbiji,Namibia,Seychelles,Zambia,Zimbabwe
na mwenyeji Tanzania,hata hivyo nchi za Botswana na Swaziland
hazitahudhulia kwakuwa ziko kwenye mchakato wa uchaguzi.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment