Mwandishi wa habari wa ITV na Radio One, Ufoo Saro, pichani, katika moja ya matukio ya kikazi hapa nchini.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MWANDISHI wa ITV na Radio One, Ufuo Saro amedaiwa kupigwa risasi ya nne za tumboni kifuani na mkononi na kupelekea kumjeruhi vibaya, huku mama yake mzazi naye akifariki baada ya kupigwa risasi katika tukio hilo.
Habari za awali zinasema kuwa mwandishi huyo pamoja na mama yake wamefanyiwa kitendo hicho na kijana aitwaye Mushi anayedaiwa kuwa ni mpenzi wa Ufoo Saro, ambaye inadaiwa alikuwa nao katika mazungumzo eneo la Kibamba nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam ndipo kijana huyo akadaiwa kuwafyatulia risasi na kisha na yeye kujiua kwa risasi.
Watu mbalimbali katika mitandao ya kijamii wameonyesha kushangazwa na tukio hilo alilofanyiwa mwanadada huyo anayefanya kazi katika kituo cha ITV na Radio One, kinachomilikiwa na Kampuni ya IPP, chini ya Mwenyekiti wake Reginald Mengi.
Blog hii inatoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki wote waliokubwa na msiba huo pamoja na kutoa salamu za pole kwa Wanahabari wote Tanzania na wafanyakazi wa IPP. Mungu amjalie afya njema na Uponyaji haraka Ufoo Saro.
Post a Comment