LOWASA AMVAA PROFESSOR SOSPETER MUHONGO:



Akihutubia katika harambee ndogo muda mfupi uliopita katika kanisa la Kipendekoste hapa Kijitonyama, Waziri Mkuu mstaafu ndugu Edward Lowassa ameonya kwamba, iwapo serikali na chama (CCM) haitafanya maamuzi magumu kuwawajibisha mawaziri wababaishaji na waropokaji kama Muhongo anayepanda mbegu za chuki, basi nchii hii itafika isitawalike na pengine tukashuhudia umwagikaji wa damu.

"Muhongo ni mtu hatari kwa usalama wa nchi hii na hatujui aliibukia wapi na kupata uwaziri, alisema Ndg. Edward Lowassa. Kauli zake zinaiweka chama, serikali na usalama wa nchi pabaya. 

Tunawaombeni makanisani muiombee hii nchi isiingie pabaya, tumesikia viongozi huko wizarani wanawatukana hadi maaskofu kuwa ni wala rushwa, wanawatukana wazalendo wanaotetea maslahi ya taifa, tunasikitika sana." Hii ni mbaya amelalamika Lowassa.Chanzo JF

Post a Comment

أحدث أقدم