Dr. Slaa anaendelea na safari yake ya kujifunza inayoitwa “Vision Tanzania” ambayo leo imemfikisha katika kituo kikubwa cha Umeme kinachoitwa Alabama Power Company ambayo inatenegenza umeme wake kutokana na jua, gesi asilia, makaa ya mawe, upepo, jua, takataka, (biomass) pamoja na nuklia

Akielezea baadhi ya shuguli za Alabama Power company, mkurugenzi wa shirika hilo linalojitegemea, ameeleza kwamba shirika hilo linawahudumia wateja million nne tu, huku ikizalisha kiasi cha megawati 48,000 (4.8GW) Tangu kuanzishwa kwa shirika hilo, hakujawahi kutokea mgao wa umeme au umeme kuzimwa hata kwa dakika 5. Panapotokea dharura, kuna kuwepo njia mbadala ya kukabiliana nayo,

Akitembelea mitambo inayopewa ulinzi wa kipekee, Dr. Slaa amejionea jinsi kampuni hiyo inavyofanya shuguli zake pamoja na kuwa na mitambo ya kisasa inayo monita njia zote za umeme kusini mwa marekani yaani, Georgia, Florida, Alabama, Mississini na South Carolina.


Dr. Slaa na ulinzi wake wakiwasili katika ofisi za Shirika la Alabama Power Company

Dr. Slaa anaelekea kwenye ofisi za shirika

Mkurugenzi mkuu akimpokea Dr. Slaa na Mkewe

Mkurugenzi wa shirika akimpa maelezo Dr. Slaa jinsi shirika hilo linavyofanya kazi

Sehemu maalum yenye ulinzi mkali ambako gridi inakuwa monitored

Dr. Slaa akitizama kwa umakini mitambo hiyo ya kusisimua inayoongoza gridi kusini mwa marekani.Hata mashine moja ikiharibika watagundua maramoja na kuweza kutafuta njia mbadala
Dr. Slaa akikabidhiwa kitabu na mwanasheria mkuu wa shirika hilo