Pages

July 7, 2013

WACHIMBAJI WATANO WAFARIKI DUNIA KATIKA MACHIMBO YA MADINI YA TANZANITE MKOA WA MANYARA


   

 
 
 
Kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara,Akili Mpwapwa amesema waliofariki dunia ni Goodlove Zablon (35) na Ndekirwa Kitoi (33) wakazi wa Makiba Wilayani Arumeru.

Kamanda  aliwataja wachimbaji wengine waliofariki ni Jackson Kavishe (45) mkazi wa Mirerani,Emmanuel John (33) mkazi wa Makiba na Emmanuel Joshua (40) mkazi wa Nkwoaranga wilayani Arumeru mkoani Arusha.

Alisema mchimbaji mwingine Sifael Simba (30) mkazi wa kijiji cha Maroroni wilayani Arumeru alijeruhiwa kwenye mbavu na tumboni ambapo amelazwa kwenye hospitali ya mkoa wa Arusha,Mount Meru.
 
 



 
   

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...