Uchaguzi wa madiwani katika Kata za Kimandolu,Elerai,Kaloleni na Themi jijini Arusha unaendelea kufanyika kwa utulivu.
Jeshi la Polisi ,Askari Magereza na Polisi walio kwenye mafunzo kutoka CCP Moshi wameonekana wakiimarisha ulinzi kwenye vituo vya kupigia kura na barabarani.
Kasoro zilizojitokeza ni baadhi ya wananchi kukosa majina yao kwenye daftari la kudumu wakati majina yao yapo ukutani na wana kadi za kupigia kura.
Pamoja na wananchi kutakiwa kuondoka kwenye vituo mara baada ya kupiga kura wananchi wengine wameonekana wakirandaranda bila sababu maalumu huku polisi wakiwa makini kuwatimua waliokua wakionekana kuwashawishi wapiga kura dakika za mwisho.
Mchuano mkali ni kati ya Chadema,CCM na CUF,bado ni mapema kubashiri chama gani jioni kitakua kikiimba nyimbo za ushindi.
endelea kufatilia.....
Mkazi wa Kaloleni akichovya kidole baada ya kupiga kura |
Askari wakiweka mambo sawa kituoni kuhakikisha usalama unadumishwa |
Ulinzi ukiwa umeimarishwa kituo cha kupigia kura |
Tunasubiri wateja jamani,wakti mwingine hali ilikua hivi kutokana na wapigakura kufika mmojammoja |
Mawakala wakihakiki majina ya wapigakura |
Mpigakura akitoa Shahada yake kwa mawakala waikague kabla ya kupigakura kwenye Kata ya Elerai Picha na www.rweyemamuinfo.blogspot.com |
No comments:
Post a Comment