PICHA NA JUMAMTANDA.BLOG
Na Esther Mwimbula,Kilosa.
WAKULIMA wa vijiji vya Mandela, Magubwige, Mabana, Mfulu, Mdudu viliyopo kata ya magole tarafa ya magole wilayani kilosa mkoani Morogoro wametakiwa kulima kilimo cha hifadhi cha mahindi na mbaazi kutokana na zao hilo kuwa na uhakika wa soko ndani na nje ya nchi.
Mtafiti wambegu za kilimo kutoka katika kituo cha utafiti cha chollima kilichopo dakawa mkoani humo Geoge Iranga alisema hayo alipokuwa akizungumza na wakulima hao na kudai kuwa imefikia wakati wakulima kulima kilimo ambacho kina manufaa kwao na kinakidhi matakwa ya wakulima.
Iranga alisema kuwaidadi kubwa ya wananchi waishio Tanzania wanategemea kilimo kwaajili ya kujikwamua kiuchumi hivyo wanatakiwa kulima kilimo ambacho kitawaingizia kipato ambacho kitawawezesha kujikwamua kiuchumi ikiwemo kuwalipia watoto wao karo za shule.
Aidha pia aliwataka wakulima hao kushiriki mafunzo mbalimbali ya kilimo cha mseto (SIMLESA)ambayo ambayo imekuwa ikiwawezesha wakulima kuweza kulima kilimo mseto ambacho kinamanufaa kwa wakulima wadogo ambao wanategemea kilimo kama msingi wa maisha yao.
Wakizungumza kwa niaba ya wakulima wenzao Jumanne Bakari na Tatu Hamis walisema kuwa kilimo mseto kimewanufaisha kiuchumi na kujikwamua na janga la njaa ambalo limekuwa ni kero wa wakulima wadogo ambao wamekuwa wakitegemea kilimo katika shughuli za kilasiku.
Hivyo waliwaomba watafiti wa mbegu na kilimo kufika maeneo ya vijijini kutoa elimu ya kutosha ili waweze kulima kilimo cha tija na kuachana na kilimo cha mazoea.

إرسال تعليق